



Sehemu ya eneo hilo ambapo litajengwa tanki la lita milioni moja za maji safi na kusambazwa Wilaya ya sumbawanga na vijiji mbalimbali mkoani Rukwa.

Mkurugenzi wa Majisafi na Majitaka Sumbawanga (SUWASA), mkoani Rukwa, Antipas Shirima akimuelekea jambo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuhusu ujenzi wa eneo la kisima cha kuchujia maji safi na hatimaye kuyapeleka kwenye matanki na baadaye kusambazwa sehemu mbalimbali za wananchi mkoani Rukwa.

Mkurugenzi wa Majisafi na Majitaka Sumbawanga (SUWASA), mkoani Rukwa, Antipas Shirima akimpatia maelezo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuhusu ujenzi wa bwawa la maji taka linalojengwa katika mradi wa SUWASA unaotarajiwa kumalizikama Machi 7, mwakani (2015). Kinana yupo mjini Sumbawanga akiwa katika ziara ya siku sita mkoani Rukwa.


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Aprili 5, 2014, katika bustani ya Uwanja wa Nelson Mandela, mjini Sumbawanga, mwishoni mwa ziara yake mkoani RukwaPicha zote na Bashir Nkoromo wa CCM Blog
No comments:
Post a Comment