
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti
na zawadi, mshindi wa kwanza kwa kulipa kodi, Meneje wa Huduma za Fedha wa
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Alois Qande Maleck, wakati wa Sherehe za
maadhimisho ya Saba ya Siku ya Mlipakodi, zilizofanyika kwenye Ukumbi wa
Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Okt 8, 2013. Kulia ni Naibu Waziri wa
Fedha, Janeth Mbene.

Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti
na zawadi, mshindi wa pili kwa kulipa kodi,Mwakilishi wa Kampuni ya Sigara
Tanzania, Paul Makanza, wakati wa Sherehe za maadhimisho ya Saba ya Siku ya
Mlipakodi, zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam,
Okt 8, 2013. Kulia ni Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene.

Mkurugenzi wa TBC BW.
Mshana akipokea Tuzo na Cheti kwa niaba ya Jukwaa la Wahariri.

Kamishna Mkuu wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania, Harry Kitilya, akimkabidhi Tuzo na Cheti, Mwananchi
Shujaa wa Kodi, Dkt. Shumba,aliyediriki kuwekwa ndani kwa kudai Risiti ya
malipo yake ya chumba cha Hoteli katika moja ya hotel katika mikoa ya Tanzania
Bara, wakati wa Sherehe za maadhimisho ya Saba ya Siku ya Mlipakodi,
zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Okt 8,
2013. Kulia ni Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Harry Kitilya,
akimkabidhi zawadi na Cheti, Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibasila, Ally
Mshana, wakati wa Sherehe za maadhimisho ya Saba ya Siku ya Mlipakodi,
zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Okt 8,
2013. Kulia ni Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene. Picha na OMR
Post a Comment