Home » » JK atua Colombo kwa mkutano wa Jumuiya Madola

JK atua Colombo kwa mkutano wa Jumuiya Madola

Written By JAK on Friday, November 15, 2013 | 4:41 AM

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjB3v6zr1KH937m77JDjcZINI27-kQwD4hQlXm-5KaLPbDVvQ3gvrGrWkodlQd7KNxe69CmGNGi89NsQuHDr8IYCghCPzcsZJTShmhloSHT2DnhSyEzR1ltInNgFw65OwbJs6-fPFtyR5lG/s640/IMG_0880.JPG
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakilakiwa kwa ngoma za kitamaduni mara baada ya kuwasili jijini Colombo, Sri Lanka, leo Novemba 14, 2013 tayari kwa mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya ya madola.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh7ED5fXveV8lSWLbtNmBPJ6Lm5FaX_-xodWwBOWzzzaCbb94mtjiJd8lyA91_y-31DLUqotwBObHXEeKk1m1ePNPpWQzBLMCtfuWovOtEXLJS-GR9_zIhaVaP7EHuz2vlEnRIn8ZIjSQM4/s640/IMG_0886.JPG


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiongea na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue mara baada ya kuwasili jijini Colombo, Sri Lanka, leo Novemba 14, 2013 tayari kwa mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya ya madola).PICHA NA IKULU
 

Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete, amewasili kwenye mji wa Colombo, Sri Lanka, tayari kwa mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola, unaoanza leo.

Rais Kikwete aliyefuatana na mkewe Mama Salma Kikwete, anahudhuria mkutano huo wa siku tatu utakaofanyika kwenye eneo la Nelum Pokuna mjini Colombo.

Mkutano huo utafunguliwa rasmi na Prince Charles, ambaye ni mtoto wa Malkia wa Uingereza na atafanya hivyo kwa niaba ya mama yake, Malkia Elizabeth.

Malkia huyo ndiye kiongozi wa Jumuiya ya Madola, ambaye hata hivyo, hataweza kuhudhuria mkutano wa mwaka huu.

Mara baada sherehe za ufunguzi, Rais Kikwete ataungana na viongozi wenzake kwa ajili ya vikao rasmi vya mkutano huo vitakavyofanyika katika Kituo cha Maonyesho ya Kumbukumbu cha Sirimavo Bandaranaike.

Miongoni mwa shughuli kubwa za leo ni pamoja na vikao viwili vya kwanza vya viongozi wa jumuiya hiyo na baadaye majadiliano.

Viongozi hao pia watahudhuria hafla rasmi ya makaribisho itakayoandaliwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Kamalesh Sharma katika Ukumbi wa Bandaranaike.

Jana Rais Kikwete na ujumbe wake, walihudhuria hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Prince Charles na mkewe.

Jumuiya ya Madola inahusisha nchi zilizokuwa chini ya ukoloni wa Uingereza na nyingine ambazo zenyewe ziliomba na kukubaliwa kujiunga nayo. Nchi hizo ni pamoja na Msumbiji na Rwanda.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger