Mhe. Anne Makinda (
Mb) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika mkutano wa mwaka
unaowakutanisha maspika na wabunge kutoka
nchi mbalimbali duniani katika
mkutano wa siku mbili unaofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Mkutano huu umeandaliwa kwa pamoja baina ya Umoja wa
Mataifa na Inter-Parliamentary Union ( IPU) katika mkutano huu pamoja na mambo mengine wabunge
wanajadiliana na kubadilisha mawazo kuhusu nafasi wa mabunge katika majadilianao yannayoendelea hivi sasa kuhusu ajenda mpaya za Maendeleo Endelevu baada ya 2015.
Kulia kwa Mhe. Spika ni
Balozi Ramadhan Mwinyi, Naibu
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
Na Mwandishi Maalum
Maspika wa Mabunge na
wabunge kutoka zaidi ya nchi mia moja
jana alhamis, wameanza mkutano wao wa mwaka wa siku mbili unaofanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, jijini New York, Marekani.
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano
huo, ambao umeandaliwa kwa
ushirikiano baina ya
Umoja wa Mataifa kupitia Baraza lake la Uchumi na Maendeleo ( ECOSOC) na
Inter- Parliamentary Union ( IPU)
unaongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda (Mb).
Mada kuu ya mkutano huu ni Re-thinking sustainable development: the
quest for a ‘ transformational’ global agenda in 2015 ambapo wabunge wamekuwa wakijadiliana na
kubadilishana mawazo kuhusu mchango wa Mabunge katika maandalizi ya Malengo
Mapya ya Maendeleo Endelevu baada ya 2015.
Mkutano umefunguliwa
na Rais wa Baraza Kuu la
Umoja wa Mataifa, Bw. John Ashe ambaye alitambua mchango wa mabunge na wabunge katika kusimamia siyo tu
utendaji wa serikali, utungaji wa sheria na sera mbalimbali na ukusanyaji wa
mapato bali pia katika kuhakikisha ustawi na maendeleo ya wananchi.
Akiwahimiza kuchagiza na kuhimiza
maandalizi ya ajenda
mpya za malengo mapya ya maendeleo endelevu.
Wengine waliozungumza
wakati wa ufunguzi wa mkutano ni Rais wa
ECOSOC Bw Nestor Osorio na Rais wa IPU
Bw. Abdelwahadi Radi
Aidha wabunge katika siku ya kwanza ya mkutano wao pia wamejadiliana na kubasilishana mawazo
na uzoefu katika mada inayohusu ‘ Jinsia kama
kitovu cha maendeleo,namna ya
kuunda malengo mapya’. Mkazo ukiwa katika kuhimiza ushiriki wa
wanawake, vijana na asasi za kiraia
Katika siku ya pili
ya mkutano utakofanyika siku ya
ijumaa, Mhe, Spika Anne Makinda ( Mb) atakuwa mmoja wa wanajopo katika mada itakayokuwa
inazungumzia utawala wa kidemokrasia na
nafasi yake katika Maendeleo endelevu.
Washiriki wengine
katika jopo hilo watakuwa ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Jan Eliasson, Balozi wa Usiswi katika
Umoja wa Mataifa, Bw. Paul Seger
na Balozi wa Costa Rica, Bw. Eduardo
Ulibarri.
Post a Comment