Home » » CUF WAZINDUA KAMPENI ZAO JIMBO LA KIEMBE SAMAKI,ZANZIBAR

CUF WAZINDUA KAMPENI ZAO JIMBO LA KIEMBE SAMAKI,ZANZIBAR

Written By JAK on Wednesday, January 22, 2014 | 10:45 PM


Na Miza Kona – Maelezo

Mwenyekiti wa chama cha Wananchi CUF Taifa Profesa Ibrahim Haruna Lipumba amewataka wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki kumchagua kiongozi atakayeweza kuingia katika bunge la katiba na kuyatetea na kuleta maslahi ya Zanzibar.

Kauli hiyo ameitoa jana huko Kiembesamaki wakati alipokuwa akizindua kampeni na kumtambulisha mgombea uwakilishi kupitia chama hicho.

Amesema kiongozi bora ni yule atakaeweza kuitetea Zanzibar na kuipatia maendeleo na kupata mamlaka yake kamili pamoja na  kuleta mabadiliko.

Aidha ameeleza kuwa CUF inataka kuleta mabadiliko katika mambo ya muungano na kuona kuwa haki inafanyika katika nchi zote.  
Aidha amesema kupita chama cha CUF wananchi watapata kiongozi mzuri atakaeweza kuingia kwenye bunge la katiba na kuitetea nchi bila ya woga wala kupoteza mwelekeo.

“Mpeleke mtu atakaeweza kuingia kwenye bunge la katiba na kutetea maslahi ya Zanzibar”, alifahamisha.

Hata hivyo amesisitiza kuwa uchaguzi ufuate utaratibu uwe huru na haki bila ya kushirikisha vyombo vyengine.

Nae mgombea uwakilishi AbdulMalik Haji Jecha amesema pindipo wananchi watamchagua ataitetea Zanzibar kwa moyo wa uzalendo na kuleta maendeleo kwa maslahi ya nchi.

Uchaguzi huo mdogo wa jimbo la Kiembesamaki unafanyika kutokana na aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo hilo Mansour Yussuf Himid kuvuliwa uwanachama kupitia CCM.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Professa Ibrahim Haruna Lipumba akimnadi mgombea wa Chama hicho katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki, Abdulmalik Haji Jecha, katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki zilizofanyika Bustani ya Kiembesamaki, Wilaya ya Magharibi Unguja.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Professa Ibrahim Haruna Lipumba na viongozi wengine wa chama hicho wakirusha mabofu kama ishara ya uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki uliofanyika Bustani ya Kiembesamaki, Wilaya ya Magharibi Unguja.
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama hicho Professa Ibrahim Haruna Lipumba katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki katika kiwanja cha Bustani ya Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi Unguja.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger