Home » » BENKI YA NMB YADHAMINI MKUTANO MKUU WA MAKAMANDA WA POLISI MOSHI

BENKI YA NMB YADHAMINI MKUTANO MKUU WA MAKAMANDA WA POLISI MOSHI

Written By JAK on Wednesday, February 19, 2014 | 10:25 PM

BENKI ya NMB imetoa kiasi cha shilingi milioni 75, kudhamini mkutano mkuu wa siku sita wa Maafisa wa Jeshi la Polisi nchini unaoendelea katika chuo cha taaluma ya Jeshi la Moshi (MPA), Mkoani Kilimanjaro. 
 Mkutano huo ambao unajumuisha makamishna, makamanda wa mikoa ya Tanzania bara na Visiwani pamoja na maafisa wakuu waandamizi wa Jeshi hilo kutoka Makao makuu, ulizinduliwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe.Pereira Sirima. 
 Akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja wa NMB, kanda ya Kaskazini, Bi. Vicky Bishubo, alisema udhamini huo unajumuisha usafiri wa mabasi kwa washiriki wote kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani, pamoja na maandalizi ya mkutano huo. 
 Alisema pamoja na hayo, NMB imetoa Kompyuta mpakato nne zitakazowezesha mipango ya Jeshi ya kupambana na Uhalifu wa Mitandao, Mikoba, Notebook na kalamu za kutosha.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Pereira Sirima akiwasili katika viwanja vya chuo cha taaluma ya polisi Moshi (MPA), kufungua mkutano mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, chuoni hapo. Mkutano huo unadhaminiwa na NMB.
Naibu waziri wa Mambo ya ndani, Pereira Sirima (katikati), IGP Ernest Mangu kulia kwake na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro katika uzinduzi wa mkutano wa Maafisa wa Jeshi la Polisi. 
Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Mhe. Pereira Sirima (katikati), akifungua mkutano huo wa Maafisa wa Jeshi la Polisi. 
Naibu Waziri katika picha ya pamoja na wadau wa Jeshi la Polisi wakiwemo wadhamini wa mkutano huo benki ya NMB.
Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Bi. Vicky Bishubo (kushoto) akifaruhia  jambo na maafisa wenzake wa benki hiyo, Meneja Mikopo  Tawi la Nelson Mandela Moshi, Saidi Pharseko,  Meneja Wateja Binafsi  Bi. Susan Shuma na Meneja Mawasiliano Bi. Josephine Kulwa.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger