Home » » DKT. BILAL AHUDHURIA MKUTANO WA NNE WA NCHI WASHIRIKI WA KANDA YA KASKAZIN, JIJINI KAMPALA UGANDA

DKT. BILAL AHUDHURIA MKUTANO WA NNE WA NCHI WASHIRIKI WA KANDA YA KASKAZIN, JIJINI KAMPALA UGANDA

Written By JAK on Friday, February 21, 2014 | 9:09 PM


  Makamu wa Rais Dkt Bilal (katikati) akizungumza na Rais wa Uganda Yower Museven (kulia) kabla ya Mkutano huo. 
Viongozi Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki wakiimba wimbo maalumu wa Afrika Mashariki, kabla ya kuanza rasmi Mkutano wa Nne wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Ushirikiano wa Kanda ya Kaskazini, uliofanyika jana kwenye Hoteli ya Speke Resort Munyonyo jijini Kampala Uganda, ambapo Tanzania imeshiriki Mkutano huo kama Mwalikwa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) na Makamu Rais wa Burundi Gervas Rufykiri, wakitia saini kushiriki katika mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) akizungumza katika mkutano huo

 Rais wa Uganda Yoweri Museven, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Nne wa wakuu wa Nchi wanachama wa Ushirikiano wa Kanda ya Kaskazini. Umoja huo unaundwa na nchi za Uganda, Kenya, Rwanda na Sudan Kusini,Tanzania na Burundi zimeshiriki mkutano huo kama nchi waalikwa ambao pamoja na mambo megine waliyojadili ni kukamilisha miradi mbalimbali inayofanywa kwa pamoja na ushirikiano huo.

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo na ujumbe wa Tanzania. 
Picha na OMR
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger