Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas akitoa elimu ya Polisi Jamii kwa viongozi, vikundi vya ulinzi shirikishi na wananchi wa Tarafa za Muklati na Enaboishu wilayani Arumeru. Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi ambaye ni Polisi Tarafa wa Muklati Elibariki Kileo akitoa taarifa kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas wakati wa makabidhiano ya kikosi kazi cha askari 15 watakaofanya kazi pamoja na wananchi wa Tarafa ya Muklati wilayani Arumeru. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi ambaye ni Polisi Tarafa wa Muklati Elibariki Kileo akitoa taarifa kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas wakati wa makabidhiano ya kikosi kazi cha askari 15 watakaofanya kazi pamoja na wananchi wa Tarafa ya Muklati wilayani Arumeru. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
MUAMKO
JUU YA ULINZI SHIRIKISHI WASHIKA KASI ARUSHA TAARIFA ZAIDI ZA UHALIFU ZATOLEWA
Na
Rashid NchimbiwaJeshi la PolisiArusha
Wananchi Mkoani hapa wameonekana kuwa na muamko zaidi
wa Ulinzi Shirikishi baada ya kutoa taarifa mbili zilizofanikisha kukamata misokoto
1,038 ya madawa ya kulevya aina ya bangi
pamoja na mirungi kilogramu 75.
Akizungumza na Waandishiwa habari ofisi kwake,
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Gilles Muroto alisema kwamba katika matukio
mawili yaliyofanikisha ukamataji wa madawa hayo taarifa zake zilitolewa na raia
wema.
Kaimu Kamanda Muroto alisema kwamba, tukio la
kwanza lilitokea tarehe 18.02.2014 muda wa saa 1:30 asubuhi maeneo ya Kituo Kikuu
cha mabasi jijini hapa ambapo mtu mmoja aitwaye Charles Ogaga Ayunga (38) raia wa Kenya na ni mkazi wa Taveta nchini humo, alikamatwa na
misokoto 1,038 ya Madawa ya kulevya aina ya bangi iliyokuwa ndani ya boksi.
Akifafanua taarifa hiyo Kaimu Kamanda huyo alisema
kwamba, siku ya tukio mtuhumiwa alikuwa anatokea maeneo ya Ngaramtoni akiwa kwenye
Hiace na alipofika maeneo ya Kituo Kikuu cha Mabasi alishuka akiwa na boksi nakutaka kupanda
basi linaloelekea Holili Wilayani Rombo lakini kabla hajapandisha boksi hilo kwenye
basi hilo watu walimshuku na kutoa taarifa katika kituo kikuu cha Polisi,
ambapo Askari waliokuwa doria maeneo ya karibu
walikwenda katika maeneo hayo na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa na misokoto
hiyo.
Mara baada
ya mahojiano mtuhumiwa alikiri kuumiliki madawa hayo ya kulevya aina ya bangi na
kueleza kwamba alikuwa anasafirisha kupeleka nchini Kenya.
Wakati
huo huo mtu mmoja aitwaye Philipo Santolin (25) Mkazi wa Holili
Wilayani Rombo alikamatwa na madawa ya kulevya aina ya mirungi yenye uzito wa kilogramu
75 ambayo ilikuwa imehifadhiwa kwenye vifurushi tofauti tofauti7.
Akifafanua tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Gilles Muroto alisema tukio hilo la ukamataji lilitokea
tarehe 19/02/2014 muda wa saa 2:00 usiku maeneo ya Kaloleni jijini hapa.
Alisema siku ya tukio wananchi walitoa taarifa katika
kituo kikuu cha Polisi kwamba, kuna mtu alikuwa anasafirisha madawa hayo katika
garia inaya Corolla lenye namba za usajili T 162 AYW toka mkoani
Kilimanjaro kuja Arusha, ndipo Askari walipoweka mtego maeneo ya Kwa Mrefu na mara
baada ya gari hilo kusimamishwa halikusimama ndipo Askari wakaamua kulifuatilia
ambapo walifanikiwa kulikamata maeneo y aKaloleni mara baada ya gari hilo la mtuhumiwa kupasuka tairi la mbele.
Kaimu Kamanda Muroto alisema mpaka hivi sasa watuhumiwa
wote wawili wanahojiwa na watafikishwa Makamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
Post a Comment