Na Abdulaziz Video, Mtwara
Kongamano kubwa la Viongozi wa Dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara
lililoandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini limeanza leo katika
manispaa ya Mtwara/mikindani kwa Viongozi hao pamoja na Waandishi wa
habari wa vyombo mbalimbali kwa kutembelea eneo la Mnazibay/Msimbati
sehemu ambayo imegundulika gesi asilia pamoja kukagua ujenzi wa eneo
la uchakataji wa Gesi hiyo.
Katika ukaguzi huo Viongozi hao wakiongozwa na Katibu Mkuu wa wizara
hiyo,Bw Eliakim Maswi baada ya kuzungukia miradi mbalimbali ya Gesi na
Mafuta kesho kutafanyika kongamano litakaloshirikisha Viongozi hao wa
Dini na Viongozi wa serikali akiwemo mkuu wa mkoa wa Lindi na Mtwara
Kauli mbiu ya kongamano hilo ni RASILIMALI ZETU ZA GESI ASILIA,MAFUTA
NA MADINI KWA AMANI NA MAENDELEO YA TAIFA.
Kongamano hilo linashirikisha zaidi ya wadau 200 kutoka mikoa hiyo ya
lindi na Mtwara wakiwemo maofisa wa wizara na serikali za mikoa hiyo
pamoja na wanahabari.
Katibu mkuu wa wizara ya Nishati
na Madini,Eliakim Maswi (wa pili kushoto) akiongozana na Viongozi wa Dini walipokuwa
wakikagua mradi wa Gesi katika eneo la Msimbati.
Baadhi ya viongozi mbali mbali wa dini wakitembelea eneo la Mnazibay/Msimbati sehemu ambayo imegundulika gesi asilia pamoja kukagua ujenzi wa eneo la uchakataji wa Gesi hiyo.
Mitambo iliyopo kwenye eneo hilo.
Ujenzi ukiendelea.
Waandishi wa habari wakiwa katika basi kuelekea eneo
la msimbati na Madimba kwa ajili ya kujionea mitambo ya gesi na ujenzi
unaoendelea katika vijiji vya msimbati na Madimba
Baadhi ya wanahabari wakiteta na Katibu mkuu wa nishati na madini mara baada ya kuwasili katika eneo la Madimba kukagua ujenzi wa sehemu ya kuchakata gesi na majumba ya wafanya kazi.
Post a Comment