Kamishna Msaidizi wa Madini ,Wizara ya Nishati na Madini , Mhandisi Hamis Komba akiongea jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Thailand Mhe. Srirat Rastapana mara baada ya kufungua maonesho ya 53 ya “Bangkok Gems & Jewelry Fair” mapema leo. Nyuma ya Kamishna ni Bw. Edward Rweymamu ni Mthamini wa Madini ya Almas Wizara ya Nishati na Madini. Kushoto Mhe. Dora Mushi mfanyabiashara wa madini kutoka Arusha.
Rais wa Shirikisho la madini ya vito na usonara la Thailand Bw. Somchai Phornchindarak akiangalia madini ya Almas katika banda la Tanzania. Anamwelekeza jambo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Vito ya Shirikisho la Wachimbaji Tanzania (FEMATA), Bw. Gregory Kibusi. Wengine wanaoshuhudia ni baadhi ya ujumbe wa Tanzania unaoshiriki maonesho hayo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA) Sam Mollel wa pili kulia akionesha Hati ya Maridhiano ya kuendeleza ushirikiano wa tasnia ya madini ya vito na usonara baada ya kusaini kati yake na Rais wa Rais wa Shirikisho la madini ya vito na usonara la Thailand Bw. Somchai Phornchindarak. Wanaoshuhudia ni Kamishna msaidizi wa Madini, Mhandisi Hamis Komba (Wa kwanza kulia) na Makamu wa Rais wa Shirikisho la madini na usonara la Thailand Bw. Peter Brooke.
Ujumbe wa Tanzania katika maonesho ya 53 ya Kimataifa ya Bangkok
katika picha ya pamoja na Rais Rais wa Rais wa Shirikisho la madini
ya vito na usonara la Thailand Bw. Somchai Phornchindarak (aliyeshika
kinyago cha mamba kilichochongwa kutokana na mawe ya madini
yanayopatikana nchini Tanzania. Kinyago hicho kimechongwa na Kituo
cha 'Tanzania Geomological Center' kilichopo Arusha.) Wa tatu kutoka
kushoto ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la madini na usonara la
Thailand Bw. Peter Brooke.
Balozi wa Afrika ya Kusini nchini Thailand Mhe. Ruby Marks (katikati)
katika picha ya pamoja na wafanyabiashara ya madini( wa kwanza
kushoto, Bw. Sam Mollel mwakilishi kutoka Tanzania Geomological Center
(wa tatu kulia) Bw. Musa Shanyangi Mwenyekiti wa Mwenyekiti wa
Kamati ya Vito ya Shirikisho la Wachimbaji Tanzania (FEMATA), Bw.
Gregory Kibusi.(nne kulia).
Post a Comment