Naibu
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya
Nje wa Japan, Bw. Norio Mitsuya, mara baada ya kuwasili katika stesheni ya Shirika la Reli Tanzania(TRL) kuangalia namna
usafiri wa Treni ya Dar es Salaam Unavyofanya kazi, leo mchana
Naibu
Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Charles Tizeba, akimuonyesha mchoro wa njia ya
treni ya Bara na ile ya inayofanya Safari zake kutoka stesheni mpaka Ubungo
Maziwa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Norio Mitsuya huku wakiwa ndani
ya treni hiyo, wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea Shirika la Reli Tanzania (TRL)
kujionea namna ya treni ya kutoka stesheni hadi Ubungo Maziwa inavyofanya kazi.
Naibu Waziri huyo ameahidi kuwa Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo
la Japan (JICA) wataendelea kuisadia miradi mbalimbali ya Reli.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Japan, Norio Mitsuya (mwenye tai ya mistari
ya Manjano) akishuka katika kituo cha Ubungo Maziwa, baada ya kumaliza ziara
yake ya kuangalia namna treni ya Dar es Salaam, maarufu kama ‘treni ya
Mwakyembe’ inavyofanya kazi leo mchana.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Charles Tizeba (wa pili kutoka kushoto), akitoa
ufafanuzi wa namna treni ya Shirika la
Reli Tanzania(TRL), inayofanya safari zake kutoka Stesheni mpaka Ubungo Maziwa inavyofanya
kazi pamoja na Matarajio ya Serikali katika kuimarisha usafiri huo kwa Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Norio Mitsuya leo mchana baada ya Naibu Waziri
wa Japan kutembelea usafiri huo na kuona namna ambavyo Serikali yake inaweza
kusaidia kuimarisha Usafiri huo. Picha
na kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi
Post a Comment