Source: Habari Leo,By Theopista Nsanzugwanko
WASOMI, wanasiasa pamoja na viongozi mbalimbali vya dini wamepongeza hotuba iliyotolewa juzi na Rais Jakaya Kikwete wakati akizindua Bunge Maalum la Katiba huku wajumbe wa bunge hilo wakitakiwa kuzingatia maoni ya Rais wanapojadili Rasimu ya pili ya Katiba hiyo.
Aidha, wamemtetea Rais kwa kutoa maoni yake kuwa ni Mtanzania mwenye dhamana na nchi, hivyo siyo mbaya kutoa mwelekeo kwa maslahi ya taifa na hajawadhibiti wajumbe kusimamia anayotaka yeye.
Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana alisema kwa ujumla hotuba hiyo ilikuwa nzuri yenye upeo na busara na yenye mambo ya msingi ili kuondoa kizungumkuti na sitofahamu kwa baadhi ya mambo.
Hata hivyo, alisema kuna mambo mengi ya msingi aliyotoa jana ambayo tume ya mabadiliko ya katiba ilitakiwa iyaingize katika rasimu ya pili.
Alisema yale yote aliyofafanua yangekuwa kwenye Tume ilikuwa ni jambo jema zaidi huku akitaka busara itumike kusoma na kuchambua hotuba ya Rais ili kuelewa maudhui na muktadha wa maneno yake.
“Ni lazima kutambua nia ya Rais katika hotuba yake kwani hakuwadhibiti wajumbe katika kufanya maamuzi, bali wanatakiwa kuwa huru kwani yale ni maoni yake yeye kama raia namba moja wa Tanzania,” alisema.
Alitaka wale wanaotaka kupinga hotuba hiyo kuleta hoja zao, kwani yeye kama Rais alitoa madukuduku yake kwa hoja na siyo kupinga kwa kejeli, kwani maoni yale ya Rais hakutoa kama mwongozo, bali wajumbe wanapojadili wayazingatie.
“Hotuba hii isije ikatafsiriwa vibaya na kuonekana kama Rais amewadhibiti wajumbe wa bunge hilo maalumu na kufanya kushindikana kupatikana katiba ya wananchi,” alisema.
Naye Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum alipongeza hotuba hiyo na kusema imeonesha watanzania dira na kuwa imefika wakati mambo yanayotatiza na yanayofaa kuwekwa wazi.
Alisema hotuba hiyo ni ukombozi wa watanzania, iliyojaa uzalendo na kujali maslahi ya taifa, hivyo lazima wajumbe wa bunge hilo maalumu kuzingatia ushauri wa Rais.
“Hotuba hii ni dira ya nchi kutokana na ufafanuzi aliotoa kuhusu suala la Muungano ambao ni nguzo kuu na Rais ana haki ya kutoa mwelekeo kama Rais wa nchi na Mtanzania kwa nia ya kuonesha njia inayofaa,” alisema.
Kwa upande wake, Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Mhashamu Method Kilaini aliunga mkono na kutoa pongezi kwa kueleza hotuba ilikuwa nzuri na kuwa alitetea vizuri msimamo alionao.
Alisema kazi iliyobaki ni kwa wajumbe wa Bunge maalumu kwa kila mmoja na dhamira yake na uhuru mbele ya Mwenyezi Mungu kutoa maoni yake atakayoona yana manufaa kwa taifa.
Naye Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba alisema Rais alitoa mawazo yake hivyo wajumbe wanatakiwa kuwa makini kuchambua na siyo kufuata yale yaliyosemwa na viongozi.
Alisema wajumbe hao wanatakiwa kufikiria sawasawa hususani wale walioteuliwa na Rais kwa kuangalia maslahi ya taifa wasifanye kama wanalipa fadhila. Mwenyekiti wa Tanzania Islamic Peace Foundation (TIPF), Shekhe Sadik Godigodi alisema hotuba ile ilikuwa na weledi wa hali ya juu, hususan katika masuala ya Muungano.
Hivyo aliwataka wajumbe wa bunge hilo kufikiria upya na kuunga mkono ushauri wa maoni na umakini mkubwa aliotoa Rais katika hotuba yake bila kuangalia kama Rais ni Mwenyekiti wa chama cha siasa bali mustakabali wa taifa.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba alisema hotuba ya Rais alikuwa akiwapa maelekezo wajumbe wa bunge hilo kwa kutumia muda mwingi kuzungumzia suala la Muungano.
Alisema Rais alionesha bayana msimamo wake na kutishika na muundo wa serikali tatu huku akipongeza kuwa aliwaelekeza wajumbe vizuri kwa nafasi yake.
Alisema jambo lingine alilopongeza ni Rais kutambua mchango wa Tume ya mabadiliko ya katiba kuwa ilifanywa kwa weledi na kubainisha kuwa kazi imebaki kwa wajumbe wa bunge hilo kufanya maamuzi.
Maoni mengine yametoka kwa wananchi wa kawaida, wakisifu na kusema sasa wana matumaini ya kupata katiba mpya yenye ubora. Wakati wengi wakisifu na kupongeza hotuba ya Rais Kikwete,
Mjumbe wa Bunge hilo Maalumu, Christopher Mtikila ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), alisema kwa hotuba yake, ni kama Rais ilimaliza mchakato wa Katiba akidai `ameikanyaga’ rasimu iliyotakiwa kujadiliwa.
Na kutokana hayo, kwa maoni yake anasema ni bora wajumbe wa Bunge wakaondoka Dodoma, akidai watakuwa wanakula posho ya bure.
Naye Julius Mtatiro, Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) upande wa Tanzania Bara, alikosoa kitendo cha Rais kutoa misimamo yake katika rasimu hiyo, akisema atasababisha wajumbe wa bunge la katiba kufuata upande wake kwa sababu wengi wa wajumbe si weledi na wachambuzi wazuri wanaweza kuibeba hotuba yake na kufuata kile alichosema.
Alisema Rais ameponda mawazo ya wajumbe wa tume ya katiba ambao wengi wanaifahamu vizuri nchi na ina maana ya kukanyaga kazi kubwa ya tume na kuyasaga maoni ya wananchi kwa imani ya chama chake.
Miongoni mwa mambo aliyoyazungumzia Rais Kikwete juzi ni juu ya muundo wa serikali tatu uliopendekezwa na Tume ya Marekebisho ya Katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba.
Katika maoni yake, Rais Kikwete alisema muundo huo hautekelezeki na kusema kero za Muungano zinaweza kutatulika kwa kuendelea na serikali mbili.
Katika hotuba yake pamoja na kuwataka wajumbe kuamua wenyewe kwa kuwa makini amesema kwamba serikali tatu kutekelezeka kwake ni kugumu kutokana na muundo wenyewe na namna ya kujipatia mapato.
Rais Kikwete alisema kutotekelezeka kwake kunatokana na serikali hiyo ya tatu kutokuwa na mapato ya uhakika, kwani haina chombo cha kukusanya mapato na badala yake inategemea nchi washirika zikusanye mapato na kuipelekea.
Alisema serikali hiyo itakuwa itegemee hisani za nchi washirika na iwapo nchi moja itaondoa hisani zake serikali ya tatu itayumba na kusisitiza;
“Kuna hatari wakati wowote serikali hiyo ya Muungano kusimama, lazima tutengeneze kitu thabiti na uwepo msingi imara.
“Serikali ya muungano ya tatu haina nyenzo wala uwezo kuhakikisha mapato yanawasilishwa. Kama tunataka kitu lazima tujipe muda tuhakikishe inasimama…rasimu inapendekeza kuweza kukopa, lakini serikali hiyo haina rasilimali na rasilimali zake ni jeshi na mizinga yake, polisi na magari yake ya washawasha, pingu na magereza yake.
“Nani hapo anakudhamini kwa rasilimali hizo? Serikali hiyo ya tatu haikopesheki labda Tanganyika iidhamini kwa sababu ina gesi, dhahabu, mtama, muhogo, mbuzi, ng’ombe na hapo asiye na kitu kinyama mwitu.
Mtasema mimi si muumini wa serikali tatu, lakini hata hao waumini wa hiyo wanajua … Wabunge wekeni sawa jinsi hiyo serikali tatu itakavyokuwa, wekeni majibu ya kukwamua matatizo yakitokea.”

Post a Comment