.jpg)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mjumbe Maalum wa Rais wa Afrika Kusini Mhe. Maite Nkoana-Mashabane, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Ikulu jijini Dar es salaam leo.
.jpg)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mjumbe Maalum wa Rais wa Afrika Kusini Mhe. Maite Nkoana-Mashabane, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nvhi hiyo Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Picha na Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,
Jumapili, Machi 16, 2014, amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Jacob Zuma wa
Afrika Kusini.
Ujumbe huo wa Rais Zuma umewasilishwa kwa Rais Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje wa
Afrika Kusini, Mheshimiwa Maite Nkoana-Mashabane wakati mama huyo alipokutana
na kufanya mazungumzo na Rais Kikwete, Ikulu, Dar Es Salaam.
Mara baada ya kuwasilisha ujumbe huo, viongozi hao wamejadili masuala yanayohusu
uhusiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini na masuala ya kikanda ambako nchi
zote mbili ni wanachama wa Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Mheshimiwa Nkoana-Mashabane ameondoka nchini mara baada ya kuwasilisha ujumbe
huo kwa Rais Kikwete.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
16 Machi,2013
Post a Comment