Home » » KINANA ATUMIA USAFIRI WA MAJINI KUINGIA MKOA WA KATAVI KUTOKEA KIGOMA

KINANA ATUMIA USAFIRI WA MAJINI KUINGIA MKOA WA KATAVI KUTOKEA KIGOMA

Written By JAK on Monday, April 14, 2014 | 5:47 AM

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgkdi6G9ztvNQS0qrWtT-r8ma6XJwrK2hlDUv52aJ7vAi6ylMQGwyhyphenhyphenW2INJdcKWr_98VFQXTr5XB6F3F62NeG6WXAvQ57VKaoKd7RJ5d3DUUUG8YQ1ToWawmpc6VYuGiPG19-n5jdCjF0o/s1600/22.jpg
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwapungia wenyeji wake (hawapo pichani) waliofika kumpokea usiku huu kwa boti akitokea mkoani Kigoma  katika bandari ya Karema mkoani Katavi,ambako amemaliza ziara yake ya siku tano na kuhamia mkoani Katavi ambako pia atakuwa na ziara ya siku nne.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEja93sg5-BdJ4XTO68urHs1VQhiCGUufvVeN0NpFgEbSOZFMrN-7yvnnyWmrrxup8NR0eJXRCyoCkrKTVgnwEgiGeaLKFEcKcHBDSKOq5jIwc8_XPS1jNDqriEInlrQb2YzoRx7PHAg5V20/s1600/26.jpg
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia kwa ufupi wakazi wa mji wa Karema mkoani Katavi usiku huu mara baada ya kuwasili akitokea mkoani Kigoma kwa boti na kusafiri nayo ndani ya ziwa Tanganyika takribani kwa masaa kumi na manne.Kutokana na safari hiyo kuwa ndefu ya majini,inaelezwa kuwa kuna baadhi ya Watu wamedai msafara wa Katibu Mkuu huyo,Kinana umepotea ziwa Tanganyika,jambo ambalo si la kweli na la kizushi.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiRp0hu6oE0XcBnKJM94tXau6QJrduoJgRvvROJewFrwt2Jegs-kU_fmDLS522owBBoqooHnpHB3Yhz0P02K3RxW2DkpJ-C8ztnUEq2sgrUy_hg1wFupMcU-Q1SyZTqJT9jrLf235yRmEKF/s1600/21.jpg
 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanal Mstaafu Issa Machibya akishuka kwenye boti usiku huu kwenye bandari ya Karema mkoani Katavi akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,na Viongozi wengine wa Taifa,Mkoa na Wilaya tayari kwa kuanza ziara ya siku nne mkoani Katavi.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgqugY-3DcSRA9gYdmIOV10PJgYjT9X1Zem-Va8sGCdZjuQfFlrEogXhO_1n0PJRemBdX3czDWDp0XROym-iCekPqigsCA-w095WkstQPjJVcMiOlZw9WqewQ6Aw2YzAYLMZxEXTUtYkSKr/s1600/23.jpg Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishuka kwenye boti wakati wenyeji wake (hawapo pichani) walipokuwa wakimsubiri kumpokea usiku huu akitokea mkoani Kigoma  katika bandari ya Karema mkoani Katavi,ambako amemaliza ziara yake ya siku tano na kuhamia mkoani Katavi ambako pia atakuwa na ziara ya siku nne.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgLaxYiqLrXa9cfGD8_BQhKbo4krejcXq2MKwj6Hd1OE0jT0yoOtr3odRxky-0qEUmX51sDFafDqma25j0d0lyvuhxDWSFAZMDIyHf2JagDPpSbpU-emmAMPea05BYYBINV3i2Dw20hNxMv/s1600/24.jpg Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa na Viongozi mbalimbali wa mkoa na Wilaya ndani ya Mkoa wa Katavi usiku huu,alipokuwa akiwasili kwenye bandari ya Karema mkoani humo usiku huu.Kinana ameongoza na Katibu Wa NEC,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye,Mjumbe wa NEC,Balozi Ali Karume,Mkuu wa mkoa wa Kigoma,Kanal Issa Machibya,Mwenyekiti wa CCM,Mkoa wa Kigoma ndugu Kabouru na wengineo.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgx7yFtnx1WwIDuH-HCLmNr0uaoawLnz_PcjRCgmvYcd2PHFv37CkgR-jsaJy7NidAOFMap0nZvAjwJRSfkx7tVBjPC02xIVAJ5DdxDJ5NAl7j1aEsMJYFTst7hYrZHsplIngcmCZ2C8CjS/s1600/25.jpg Kinana akipokelewa na Gwaride la chipukizi usiku huu ndani ya mkoa wa Katavi.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger