Home » » MAMA YAKE MZAZI WAZIRI MKUU MH. PINDA ATEMBELEWA NA KATIBU MKUU WA CCM NDG KINANA NYUMBANI KWAKE.

MAMA YAKE MZAZI WAZIRI MKUU MH. PINDA ATEMBELEWA NA KATIBU MKUU WA CCM NDG KINANA NYUMBANI KWAKE.

Written By JAK on Tuesday, April 15, 2014 | 8:33 PM



Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na Mama Mzazi wa Waziri Mkuu,Mh Pinda, mapema mchana huu nyumbani kwake,Katika kijiji cha Kibaoni Wilaya Mlele mkoani Katavi,alipokwenda kumtembelea na kumjulia hali.Kinana yuko Mkoani Katavi kwa ziara ya siku nne ya kuimarisha uhai wa chama,kukagua na kuhimiza ilani ya Uchaguzi ya 2010.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mama Mzazi wa Waziri Mkuu,Mh Pinda, mapema mchana huu nyumbani kwake,Katika kijiji cha Kibaoni Wilaya Mlela mkoani Katavi,alipokwenda kumtembelea na kumjulia hali.

Kinana akijaribu kuelewesha jambo katika shamba la Ufugaji nyuki la Waziri Mkuu Pinda,katika kijiji cha Kibaoni Wilaya ya Mlele mkoani Katavi mapema leo mchana

Kinana akikatiza kwenye Shamba la Ufuta na Nyuki mara baada ya kujionea ufugaji wa nyuki unavyofanyika.

Katibu Mkuu wa CCM,akikagua Ujenzi wa Mradi wa Maji safi,katika kijiji cha Kibaoni,Wilaya ya Mlele,mkoani Katavi.Tanki hilo la maji safi linatarajia kuhudumia wakazi wa kijiji cha Kibaoni na vijiji vingine tisa.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger