Home » » MIAKA 50 YA MUUNGANO UWANJA WA TAIFA

MIAKA 50 YA MUUNGANO UWANJA WA TAIFA

Written By JAK on Monday, April 28, 2014 | 12:53 AM



Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia wananchi wakati alipokuwa anaingi uwanja wa Uhuru leo katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar..Pembeni ni Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam .

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Joyce Banda wa Malawi katika sherehe za miaka 50 ya Muungano.Rais Banda kwa sasa ndiye mwenyekiti wa jumuiya ya uchumi kusini mwa Afrika SADC.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt.Mohamed Ali Shein wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya muungano.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Mfalme MswatiIII katika sherehe za miaka 50 ya Muungano zilizofanyika katika viwanja vya uhuru .

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Yoweri Kaguta Museveni katika sherehe za miaka 50 ya Muungano.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi katika maadhimisho ya hsrehe za miaka 50 ya Muungano.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Uhuru Kenyatta katika hsrehe za miaka 50 ya Muungano.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Mohamed Ali Shein na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakiwa na viongozi wa nchi mbalimbali za Afrika kwnyesherehe za Miaka 50 ya Muungano katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo. Wengine toka kushoto ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi, Mfalme Mswati wa III

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal, Mfalme wa Lesotho na rais wa Malawi Dkt Joyce Banda. na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakiwa na viongozi wa nchi mbalimbali za Afrika kwnyesherehe za Miaka 50 ya Muungano katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam .

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal,  na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakishyangilia kwa furaha wakati Makomandoo wakishuka kwa miavuli uwanjani kama inavyoonekana hapo chini.

Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger