Home » » NDG,KINANA AKAGUA MIRADI YA MAJI TAKA NA MAJI SAFI WILAYANI SUMBAWANGA MKOANI RUKWA LEO.

NDG,KINANA AKAGUA MIRADI YA MAJI TAKA NA MAJI SAFI WILAYANI SUMBAWANGA MKOANI RUKWA LEO.

Written By JAK on Saturday, April 5, 2014 | 10:16 PM



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgW-AL0Z82P3iMNLCtXwX7Zp626vxEHew3djYu7xcurj6DPvMzOsJB3731WVGVr-8M5pfls6B85xXgWhfdvnKLZKMMVcd00wFmuDsJAk0PePGLe1GeDle5qDG8_O_Rfe6EQBm8LPOheueA6/s1600/IMG_3498.jpg
Mkurugenzi wa Majisafi na Majitaka Sumbawanga (SUWASA), mkoani Rukwa, Antipas Shirima akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana kuhusu ujenzi wa tanki la lita milioni moja za majisafi linalojengwa katika mradi wa SUWASA unaotarajiwa kumalizika Machi 7, mwakani (2015). Mradi huo mpaka unakamilika utagharimu kiasi cha fedha shilingi Bilioni 30.Pamooja na kutembelea mradii wa maji safi,Kinana pia alitembelea mradi wa maji taka wilayani humo mapema leo.Ndugu Kinana anamaliza zaira yake leo ya siku sita mkoani Rukwa.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiI3vdA4UeiEpFGsrbnySwpg2KJ5Jp3OZ9zhSLL7Z6Y4ll0pw_SeX6ne4hmjYVrUOyz5nzbd2oGHtEKXbbNyrnLqobxZdbZny5Pav1-1vyCJbHIHwOIP8bh2Fme98mSEeVOwRGmztvMs-L9/s1600/IMG_3506.jpg
Sehemu ya eneo hilo ambapo litajengwa tanki la lita milioni moja za maji safi na kusambazwa Wilaya ya sumbawanga na vijiji mbalimbali mkoani Rukwa.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhGfM9zu03Rmcm9NtR0s1KRba-ExfsDOyfVvp6Gywv91Cor1BxmqRiDPjWj4c4CxhBktkTCYATGiPofuaCK9UzDpO1ihcoFsrp9VyGmKQ95aaq8x4sqZl6E_7nMvf5Ff0EqN_WANgJZvzW-/s1600/IMG_3537.jpg
Mkurugenzi wa Majisafi na Majitaka Sumbawanga (SUWASA), mkoani Rukwa, Antipas Shirima akimuelekea jambo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuhusu ujenzi wa eneo la kisima cha kuchujia maji safi na hatimaye kuyapeleka kwenye matanki na baadaye kusambazwa sehemu mbalimbali  za wananchi mkoani Rukwa.


 Mkurugenzi wa Majisafi na Majitaka Sumbawanga (SUWASA), mkoani Rukwa, Antipas Shirima akimpatia maelezo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuhusu ujenzi wa bwawa la maji taka linalojengwa katika mradi wa SUWASA unaotarajiwa kumalizikama Machi 7, mwakani (2015). Kinana yupo mjini Sumbawanga akiwa katika ziara ya siku sita mkoani Rukwa.
Kinana akionyeshwa mtandao wa huduma za usambazaji maji Sumbawanga utakavyokuwa. Anayempa maelezo ni Ngainayo Colman wa SUWASA. 

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Aprili 5, 2014, katika bustani ya Uwanja wa Nelson Mandela, mjini Sumbawanga, mwishoni mwa ziara yake mkoani RukwaPicha zote na Bashir Nkoromo wa CCM Blog
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger