Rais mpya wa TFF Jamal Malinzi akiwa na Dream Team yake
baada ya uchaguzi
Rais Mstaafu wa TFF LEodegar Chilla Tenga akimkabidhi mikoba
Rais Mpya Jamali Malinzi akkisaidiwa na katibu mkuu Angetille Osiah.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini aliyemaliza muda
wake,Leodger Tenga (kushoto) akimkabidhi Mpira Rais Mpya wa shirikisho
hilo,Jamal Malinzi mara baada ya kutangazwa mshindi katika Uchaguzi uliofanyika
jana na kumalizika usiku wa kuamkia leo,ambapo alimshinda mpinzani wake,Athuman
Nyamlani kwa kura 73.uchaguzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Water
Front jijini Dar es salaam.Katika uchaguzi huo nafasi ya Umakamu wa Rais
ilichukuliwa na Walace Karia ambaye alifanikiwa kuwagaragaraza wapinzani wake
Imani Madega na Ramadhan Nassib.
Rais Mpya wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini,Jamal
Malinzi akizungumza machache na Wajumbe
wa Uchaguzi huo mara baada ya kutangazwa Mshindi wa nafasi ya Urais wa TFF,usiku wa kuamkia
leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Water Front,jijini Dar es Salaam.Kulia ni Makamu Mpya wa
Rais wa TFF,Walace Karia.
wa Uchaguzi huo mara baada ya kutangazwa Mshindi wa nafasi ya Urais wa TFF,usiku wa kuamkia
leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Water Front,jijini Dar es Salaam.Kulia ni Makamu Mpya wa
Rais wa TFF,Walace Karia.
Rais Mpya wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini,Jamal
Malinzi akipongezana na Makamu Mpya wa
Rais wa TFF,Walace Karia mara baada ya kuibuka Kidedea.
Rais wa TFF,Walace Karia mara baada ya kuibuka Kidedea.
Shangwe,Nderemo na Vifijo vilitawala kwenye eneo la Ukumbi
wa Water Front jijini Dar es Salaam,mara baada ya Washindi kupatikana.
UPIGAJI KURA
Jamal Emil Malinzi ndiye Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) baada ya kuibuka kidedea katika uchaguzi mkuu wa
shirikisho hilo kwa kupata kura 73 kati ya kura 126 zilizopigwa, dhidi ya
mpinzania wake Athumani Nyamlani aliyepata kura 52 kwenye kinyang'anyiro hicho kilichohitimishwa
usiku wa kuamkia leo katika jengo la NSSF la Waterfront jijini Dar es salaam.
Malinzi ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha soka cha mkoa
wa Kagera ameshinda uchaguzi huo ikiwa ni mara yake ya pili kugombea baada ya
kushindwa na Rais wa zamani wa TFF Leodgar Chillah tenga mwaka 2008.Nafasi ya
Makamu wa Rais imenyakuliwa na Wallace Kiria aliyemshinda Ramadhani Nasib kwa
kura 67 dhidi ya 52, wakati mgombea mwingine katika nafasi hiyo Imani Mahugila
Madega kapata kuta 6.
Katika nafasi za Ujumbe; Kanda ya 13; kiungo wa zamani wa
Simba SC Wilfred Kidau amepata kura 60 na kuwashinda Muhsin Said kura 50, Omar
Abdulkadir kura 10 na Alex Kabuzelia kura nne.
Kanda 12; Khalid Mohamed Abdallah amepata kura 69 na
kumshinda Davies Mosha aliyepata kura
54.
Kanda ya 11 Geoffrey
Nyange ‘Kaburu’ amepata kura 78 na kuwashinda Riziki Majala kura tano, Twahir
Njoki kura mbili, Juma Pinto kura 26 na Farid Mbaraka kura 14, Kanda ya 10
ameshinda Hussein Mwamba aliyepata kura 63, huku Charles Komba akipata nne na
Stewart Nasima 58.
Kanda ya tisa Othman
Kambi aliyepata kura 84 yeye amewashinda Francis Bulame kura 30, wakati James
Mhagama aliyepata 93 amemshinda Zafarani Damoda aliyepata kura 11 na Kanda ya
nane, Ngube Kiondo amepata kura 73 amemshinda Ayoub Nyaulingo kura 52.
Kanda ya Tano, Ahmed
Iddi Mgoyi aliyepata kura 92 amemshinda Yussuf Kitumbo aliyepata kura 34,
wakati Kanda Omar Walii Ali amepata kura 53 dhidi ya 19 za Ally Mtumwa.
Eley Mbise amepata kura 51 dhidi ya 53 kura 57 za Lamanda
Swai.
Mbasha Matutu aliyepata kura 63, amembwaga Vesastis Ligano
aliyepata kura 61, wakati Vedastus Lufano aliyepata kura 51, amewashinda Jumbe
Odesa Magati kura 11, Mugisha Galibona kura 24 na Samuel Nyalla kura 39 na
Kanda namba moja, Karilo Samson hakuwa na mpizani akapita moja kwa moja.
Picha na
FullShangwe Blog.
Post a Comment