Home » » MOBILE BANKING YA BENKI YA NBC ARUSHA - TANZANIA

MOBILE BANKING YA BENKI YA NBC ARUSHA - TANZANIA

Written By JAK on Tuesday, October 29, 2013 | 1:16 AM

 
Mkurugenzi. mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Mwelu (kushoto), akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, John Mongela wakati mkurugenzi huyo alipometembelea mkuu huyo wa mkoa kwa lengo la kufahamiana, jijini Arusha.



Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu (kulia), akimsikiliza Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha na ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, John Mongela wakati mkurugenzi huyo alipofika kwenye ofisi za mkuu wa mkoa huyo kujitambulisha. Katikati ni Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa NBC,William Kallaghe. Bi. Mizinga pamoja na kujitambulisha lakini pia alielezea mipango na mikakati ya NBC kwa mkuu huyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania , Mizinga Melu (kushoto) akimwelekeza mmoja wa wateja wa benki hiyo, Hangi Donald Kiloba, jinsi ya kupata huduma za kibenki za NBC kwa kupitia mitandao ya simu za mkononi (NBC Mobile Banking) kwenye tawi la benki hiyo la Uhuru jijini Arusha mwishoni mwa wiki. Wateja wa NBC wanashauriwa kuendelea kwenda katika matawi ya benki hiyo nchini kote kuunganishwa na huduma hiyo. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (kulia) akimsalimia mmoja wa wateja wa benki hiyo, Christopher Cyprian katika tawi la NBC la Uhuru jijini Arusha. katikati ni Meneja wa tawi hilo, Aliko Mwamusaku . Mkurugenzi aliwambia wateja tawini hapo kujiunga na huduma za kifedha za NBC kwa kutumia mitandao ya simu za mkononi (NBC Mobile Banking) ili kupata huduma za kibenki na pia kufanya malipo ya huduma mbalimbali kutoka kwa watoa huduma watakaounganishwa na NBC Mobile banking.
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Uhuru mkoa wa Arusha, Aliko Mwamusaku (kushoto) akimtambulisha Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Mizinga Melu (katikati) kwa mmoja wa wateja wa benki hiyo Sijohn Chembakassery wakati wa ziara ya mkurugenzi huyo tawini hapo jijini Arusha.
Na Michuzi Blog
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger