YA KUCHANGISHA FEDHA ZA UJENZI
WA SHULE ZA SEKONDANI ZA KATA KATIKA TARAFA YA MBAGALA,JIJINI DAR
Brass Band ya Jeshi
la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ikiongoza Matembezi ya Hisani kwa ajili ya
Harambee ya Kuchangisha fedha za Ujenzi wa Shule za Sekondani za Kata katika
Tarafa ya Mbagala,iliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Mt.
Anthony,Mbabala jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Mgeni Rasmi katika
Harambee hiyo ambayo iliambatana na Uzinduzi wa Mahafali ya Wanafunzi wahitimu
wa Kidato cha Nne alikuwa ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la
Monduli,Mh. Edward Lowassa.ambapo zaidi ya shilingi milioni 250 zilipatikana
kwenye harambee hiyo.
Baadhi ya Askari wa
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakipiga vyombo mbali mbali vya Muziki
kwenye Matembezo hayo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward
Lowassa (katikati) ambaye ndie aliekuwa Mgeni Rasmi kwenye harambee hiyo
akionekana kwenda sambamba na Matembezi hayo.
Mh. Lowassa
akiwasalimia Wanafunzi,Walimu na Wazazi wa Watoto wanaosoma katika Shule mbali
mbali za Sekondari eneo la Mbagara jijini Dar es Salaam leo.
Sehemu ya Wanafunzi
kutoka Shule mbali mbali za Kata zilizopo kwenye Tarafa ya Mbagala jijini Dar
es Salaam wakimsikiliza Mgeni Rasmi,Mh. Edward Lowassa (hayupo pichani).
Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza wa Shule ya Sekondari ya
Mbagala jijini Dar es Salaam,Kijoy Selemani akisoma Risala ya Wanafunzi kwa
niaba ya Wenzake wa Shule mbali mbali zilizopo katika Tarafa ya Mbagala jijini
Dar es Salaam,wakati wa Harambee ya Kuchangisha fedha za Ujenzi wa Shule za
Sekondani za Kata katika Tarafa ya Mbagala iliyoenda sambamba na Uzinduzi wa
Mahafali ya Wanafunzi wahitimu wa Kidato cha Nne,iliyofanyika katika Uwanja wa
Shule ya Sekondari ya Mt. Anthony,Mbabala jijini Dar es Salaam
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward
Lowassa akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Mh. Dkt. Faustine
Ndugulile muda mfupi kabla ya kuanza kwa harambee hiyo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbagala,Mwl. Marcelina
Kimario akisoma risala mbele ya Mgeni Rasmi kwenye Harambee hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Mh. Dkt. Faustine Ndugulile
akiwahutubia Wananchi wa Mbagala pamoja na Wanafunzi wa Shule mbali mbalia
zilizopo kwenye Tarafa ya Mbagala,wakati wa Harambee ya Kuchangisha fedha za
Ujenzi wa Shule za Sekondani za Kata katika Tarafa ya Mbagala iliyoenda
sambamba na Uzinduzi wa Mahafali ya Wanafunzi wahitimu wa Kidato cha
Nne,iliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Mt. Anthony,Mbabala
jijini Dar es Salaam
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward
Lowassa akiwahutubia Wananchi wa Mbagala pamoja na Wanafunzi wa Shule mbali
mbalia zilizopo kwenye Tarafa ya Mbagala,wakati wa Harambee ya Kuchangisha
fedha za Ujenzi wa Shule za Sekondani za Kata katika Tarafa ya Mbagala
iliyoenda sambamba na Uzinduzi wa Mahafali ya Wanafunzi wahitimu wa Kidato cha
Nne,iliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Mt. Anthony,Mbabala
jijini Dar es Salaam.ambapo jumla ya Sh. Mil 250 zilipatikana kwenye harambee
hiyo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward
Lowassa akisalimina na Mbumge wa Jimbo la Ilala,Mh. Mussa Azan Zungu.
Wananchi wa Mbagala wakionyesha moyo wao wa kuchangia elimu
katika Tarafa yao,mbele ya mgeni rasmi.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward
Lowassa akizungumza jambo na mmoja wa wakazi wa Mbagala aliejitambulisha kwa
jila la Bi. Aisha.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward
Lowassa akikabidhi vyeti vya kuhitimu elimu ya Sekondari kwa wanafunzi wa
Kidato cha Nne kutoka shule mbali mbali zilizopo kwenye tarafa ya Mbagala
jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Madiwani wa Temeke wakiwa kwenye Harambee hiyo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward
Lowassa (katikati) akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee
hiyo,Bw. Tryphon Lutina (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa harambee
hiyo.Kushoto ni Mbumbe wa Jimbo la Kigamboni,Mh. Dkt. Faustine Ndugulile.
Picha ya Pamoja na wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya
harambee hiyo.
Mh. Lowassa akiwaafa wakazi wa Mbagala.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward
Lowassa akiagana na Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Mh. Dkt. Faustine Ndugulile.
by MUHIDIN MICHUZI
Post a Comment