Home » » MTANZANIA KUWANIA UBINGWA WA DUNIA WA WBC KWA MARA YA KWANZA

MTANZANIA KUWANIA UBINGWA WA DUNIA WA WBC KWA MARA YA KWANZA

Written By JAK on Thursday, October 31, 2013 | 9:29 AM



 Omari Kimweri

BONDIA MTANZANIA    Omari Kimweri 'Lion Boy' anaefanya shughuli zake Deer Park, Victoria, 

nchini Australia anatarajia kuwa mtanzania wa kwanza kupanda ulingoni kugombea ubingwa wa Dunia unaotambuliwa na  WBC uzito wa kg47.5minimum weight.

 


Mpambano huo utakaopigwa nchini China   November 30, 2013   Mchina Xiong Zhao Zhong 

ambaye ni bingwa wa dunia wa WBC ambaye anashikilia taji hilo kwa sasa katika uzito huo


Kimweri anakuwa mtanzania wa kwanza kuwania taji kubwa kabisa Duniani akitokea nchini Austalia.


Omari Kimweri na Randy petalcoria


 


Kigezo cha kufanya apate pambano hilo kubwa ni kutokana na rekodi yake pamoja na kutakiwa mtu ambaye anatokea bara la Afrika ambapo kura imemdondokea bondia Omari Kimweri, ambapo ni kiu ya mabondia wengi duniani kumiliki mikanda mikubwa ya kimataifa. Kimweri mwenye rekodi  ya kucheza michezo 16 ambapo ameshinda michezo 13 na kuchezea kichapo michezo 3  wakati mpinzani wake   Xiong Zhao Zhong amecheza michezo 26 akishinda 21 kupigwa 4 na kutoka droo moja.


 


Mabondia hao wote wana umri wa  miaka 31, wakitofautiana kwa mwezi mmoja tu katika kuzaliwa. Mpambano wao umekuwa gumzo katika dunia ambapo kila mmoja anajiandaa kwa nguvu


Kimweri kwa sasa anaefanya mazoezi makali, akipewa sparring na bondia  Randy Petalcoria  wa 

Philippines ambaye ni bingwa wa  light fly weight.

 Omari Kimweri kwa sasa yupo katika mazoezi mazito ya kujiandaa na mpambano huo, akitegemea


 zaidi dua za Watanzania kwa kuwa ushindi wake ni ushindi wa watanzania wote.


 Mungu Ibariki Tanzania 


Mungu Mbariki Bondia Omari Kimweri

Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger