Picha ya ramani ya kiwanda kitakavyokuwa ikikamilika kazi ya
Ujenzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Meis Merey Ally Saleh akimpokea Dr
Rashid aliyetembelea kukagua kazi za ujenzi wa kiwanda cha saruji mjini Lindi.
Mhandisi Rashid wa Sharjah alievaa kilemba akiangalia mchoro
wa ujenzi alipokuwa akikaua eneo la Ujenzi ambapo Mkurugenzi wa Meis na Meneja
wake wakitolea maelezo.
Majengo na kazi inavyoendelea ya ujenzi wa kiwanda hicho.
Na
Abdulaziz Lindi
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Bandari ya Nchi ya Sharjah UAE, Mhandisi Rashid Al Leem
amefurahishwa na hatua ya Kampuni ya Meis kuanza kwa kasi ujenzi wa kiwanda cha
saruji katika wilaya ya Lindi huku akiutaka uongozi wa kiwanda hicho kuongeza
juhudi ili kukamilisha kwa wakati kama ilivyokusudiwa ili mji huo uongeze ajira
hali itakayosaidia kuinua Uchumi.
Alibainisha
hayo alipokuwa akiongea na globu hii muda mfupi baada ya kukamilisha ziara yake
ya kukagua Ujenzi wa Kiwanda hicho alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea wilaya
hiyo baada ya kukutana na Serikali ya Zanzibar ambapo aliahidi Kuwekeza katika
nyanja mbalimbali.
Dr
Rashid alisema kukamilika kwa kiwanda hicho kutasaidia kuongeza kiwango cha
ajira, kipato cha wananchi wa kawaida wa mkoa wa Lindi na Taifa kwa jumla na
kupunguza gharama za ujenzi wa makazi kwa kupata saruji kwa bei ya chini na kwa
ukaribu kuliko ilivyo sasa.
“Kukamilika
kwa ujenzi wa kiwanda hiki itakuwa ni fursa ya pekee kwa wakazi wa mikoa ya
kusini kupata saruji kwa bei nafuu na ajira kwa vijana wa mikoa hii ambapo Nchi
yetu imeamua kutaka kuwekeza ndio maana pia nitatembelea Bandari ya Mtwara.
Kwa
upande wake meneja wa mradi huo, Valerian Magembe alisema ujenzi wa kiwanda
hicho umefikia hatua mzuri kwani mitambo yenye thamani ya dola za kimarekani
milioni 25 kutoka nchini China inatarajiwa kuwasili hivi karibuni baada ya
kupakilwa huko shanghai,
“Mitambo
inayotarajia kuwasili ni mitambo mizito yenye cbm 6200 ya kusaga
mawe,kunyangia, kutenganisha, pamoja kuweka dawa,kuumua na kuunda simenti na
kwa sasa tayari imepakiwa kwenye meli toka Shaghahi, China na ipo safarini
itawasili muda wowote kuanzia sasa ”alisema Magembe.
Aliongeza
kuwa ujenzi wa kiwanda hicho uko kwenye hatua ya kusaga mawe baada ya kufanya
kazi kubwa ya kukata mlima ili kufanya eneo hilo liwe tambarale.
“Kazi
kwenye eneo ilikuwa ngumu kwani lina miinuko mikubwa hata hivyo sehemu kubwa tumeikamilisha
na tupo hatua za mwisho”alibainisha Magembe.
Aidha
ujezi wa kiwanda cha sementi Lindi ulinza mwezi februari mwaka 2013 na
unatarajia kukamilika septemba 214 na kuajiri watu zaidi 2000 pamoja na
kuzalisha tani 20000 kwa siku na kuongeza kipato kwa wakazi wa mkoa wa Lindi.
Katika
ziara hiyo Dr Rashid aliongoza ujumbe toka Serikali ya Sharjah huku akiwemo
Balozi wa Comoro Nchini Balozi Islam Ally Saleh ambapo pia msafara ulitembelea
makazi ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa,Bernard Membe
kijijini Rondo wilayani humo
Post a Comment