MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA
HIFADHI YA MAZINGIRA WA VIKUNDI VIDOGO VYA UCHAKATAJI MAWESE IGALULA MKOA WA
KIGOMA JANA.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia na
kusikiliza maelezo kuhusu maandalizi ya jinsi ya kukamua mafuta ya Mawese
kutoka kwa Meneja wa mradi wa Hifadhi ya Mazingira ya Ziwa Tanganyika, Seleboni
John Mushi, wakati Makamu alipozindua mradi huo jana Igalula, Wilaya ya Uvinza
Mkoa wa Kigoma. Dkt. Bilal, alitembelea na kukagua mradi huo unaosimamiwa na
Ofisi yake na kujionea jinsi mafuta hayo yanavyopatikana. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la
Msingi katika Mradi wa Hifadhi ya Mazingira wa Vikundi vidogo vya Uchakataji
Mawese Igalula Mkoa wa Kigoma, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jana Wilayani
Uvinza. Kulia ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula. Mradi huo
unasimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu ukamuaji wa mafuta ya Mawese
Kaimu Meneja wa kutoka kwa Meneja Sido Mkoa wa Kigoma, Gervas Ntahamba, wakati
wa hafla ya uzinduzi wa mradi huo iliyofanyika jana Igalula, Wilaya ya Uvinza
Mkoa wa Kigoma. Dkt. Bilal, alitembelea na kukagua mradi huo unaosimamiwa na
Ofisi yake na kujionea jinsi mafuta hayo yanavyopatikana.
Post a Comment