Home » » WATANZANIA 3 WATIWA MBARONI WAKIWA NJIANI KWENDA KUJIUNGA NA AL-SHABAAB NCHINI SOMALI

WATANZANIA 3 WATIWA MBARONI WAKIWA NJIANI KWENDA KUJIUNGA NA AL-SHABAAB NCHINI SOMALI

Written By JAK on Friday, October 25, 2013 | 1:40 AM


Baadhi ya wanamgambo wa kikundi cha Al-Shabaab.
Jeshi la Ulinzi la Kenya liliwatia mbaroni Watanzania watatu ndani ya Somalia wakiwashuku kuwa walikuwa njiani kwenda kujiunga na Al-Shabaab, gazeti la The Standard la Kenya liliripoti siku ya Jumapili (tarehe 20 Oktoba).
Ali Ramadhan mwenye umri wa miaka 22, Musa Daudi miaka 19 na Shabaan Bakiri Waziri miaka 21, walitiwa mbaroni baada ya kuingia Somalia kutoka Kenya na sasa wanahojiwa katika kituo cha polisi cha Kiunga.
Polisi walisema kwamba washukiwa hao walitokea Dar es Salaam, wakasafiri hadi mpaka wa Tanzania na Kenya huko Lungalung, baadaye wakaenda kwa gari hadi Mombasa, Malindi na Lamu kabla ya kuingia Somallia.
Kwa mujibu wa polisi, watatu hao walikuwa wanaelekea Kismayu kwenda kujiunga na "vita vitakatifu, walivyodai vinaongozwa na [Al-Shabaab]
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger