Kundi
moja ambalo lilikuwa likicheka huku wakimlowesha mwanamke mmoja kwa
tindikali wakati mama huyo akiwasindikiza nyumbani watoto wake mapacha
wenye miaka sita kutoka shuleni, wamehukumiwa kifungo cha jumla ya miaka
44 jela.
Washambulizi
hao walisikika wakicheka huku kimiminika hatari kikifukiziwa kwa mama
huyo aliyekuwa akipiga kelele za uchungu mbele ya watoto wake wawili wa
kiume nje ya Shule ya Msingi ya Upton Cross mjini Upton Park, mashariki
mwa London.
Akizungumza
baada ya shambulio hilo mwanamke huyo, ambaye aliungua vibaya usoni na
mwilini mwake, alisema: "Nilimwona mwanaume akinikabili ambaye alikuwa
amebeba kitu fulani ndani ya chupa.
"Alinirushia na baada ya sekunde chache ikaanza kuniunguza. Nilikuwa nikilia: "Tafadhali nisaidieni! Tafadhali nisaidieni!"
Inadhaniwa Yannick Ntesa,
mwenye miaka 25, alifukiza tindikali hiyo na kutoweka ndani ya gari lake
aina ya BMW lenye rangi nyekundu akiwa na Abdul Motin, miaka 28, na
Ahad Miah mwenye miaka 31.
Mama huyo mwenye miaka 44,
kutoka Plaistow, alikimbilia kwenye nyumba moja ya jirani ambako maji
yalimwagiwa kwenye nguo zake zilizokuwa zikiungua.
Baadhi ya tindikali iliunguza
mkoba wa mtoto wake wakatimama mwingine pia alipata majeraha madogo
katika shambulio hilo lililotokea Machi 24, 2011.
Muathirika huyo alikimbizwa
katika Hospitali ya Royal London na baadaye akahamishiwa kwenye kitengo
cha mtaalamu mmoja wa majeraha ya moto huko Chelmsford, Essex.
Ameathirika asilimia 16 ya kuunguzwa na kemikali hiyo na bado anapatiwa matibabu.
Kufuatia kesi iliyochukua wiki
sita kwenye Mahakama ya Blackfriars korti imewatia hatiani Ntesa, Motin
na Miah kwa shambulio la kudhuru mwili na kumrushia mwingine kimiminika
hatari kwa kudhamiria.
Motin, kutoka Stepney, mashariki mwa London, alihukumiwa kifungo cha miaka 16 jela.
Ntesa, kutoka Paddington, na Miah, ambaye hana makazi maalumu, wote walihukumiwa kifungo cha miaka 14 jela.
Hakuna sababu yoyote ya
shambulio hilo iliyotolewa lakini Inspekta Mpelelezi John Reynolds, wa
Ofisi ya Upelelezi ya Newham, alisema: "Hakika hili ni shambulio ya
kushitusha kwa mama ambaye alikuwa na watoto wake wadogo mno wawili
sambamba nao wakati huo.
Naomi Oni, mwenye miaka 21,
ambaye alikuwa akifanya kazi Westfield Shopping Centre huko Stratford,
alikaa mwezi mzima hospitalini baada ya shambulio la tindikali huko
Dagenham, Essex, saa za mapema Desemba 30, mwaka jana.
Mnamo Aprili, mwanamke mmoja
aliyetambuliwa kama Tara, alimwagiwa tindikali usoni baada ya
kumfungulia mlango mgeni nyumbani kwake huko Romford.
Post a Comment