Home » » WATUHUMIWA WA MAUAJI YA MFANYA BIASHARA WA MADINI YA TANZANITE WA JIJINI ARUSHA WAFIKISHWA MAHAKAMANI

WATUHUMIWA WA MAUAJI YA MFANYA BIASHARA WA MADINI YA TANZANITE WA JIJINI ARUSHA WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Written By JAK on Tuesday, October 29, 2013 | 2:01 AM



 
Mshitakiwa, Sharif Mohamed Athuman (31), ambaye ni mshitakiwa namba moja katika kesi ya Mauaji ya Bilionea wa Madini ya Tanzanite, Erasto Msuya mchimbaji mdogo wa madini na mkazi wa Kimandolu mkoani Arusha, akitoka nje ya Mahakama ya Hakimu mkazi Moshi, muda mfupi baada ya kesi hiyo kuahirishwa hadi Desemba 11, mwaka huu.
 
Mshitakiwa namba mbili, Shaibu Jumanne Saidi maarufu kama Mredi (38),anayetuhumiwa na wengine saba, kumuua Mfanyabiashara Erasto Msuya kwa kumpiga risasi akitoka kwa taabu nje ya mahakama ya Hakimu mkazi Moshi, baada ya kesi hiyo kuahirishwa hadi Desemba 11, mwaka huu.
 
Mmoja wa Washtakiwa katika kesi ya Mauaji, anayetuhumiwa kushirikiana na wenzake saba, kumuua Mfanyabiashara Erasto Msuya kwa kumpiga risasi akisindikizwa na Maaskari kutoka katika mahakama ya Hakimu mkazi Moshi, muda mfupi baada ya kesi hiyo jana kuahirishwa hadi Desemba 11,mwaka huu.
 
Washitakiwa Joseph Damian "Chusa" na mwenzake Shaibu Jumanne Saidi "Mredi", wakimsaidia Mshitakiwa mwenzao kupanda katika Gari la Polisi muda mfupi baada ya kesi inayowakabili ya mauaji ya Bilionea wa Madini ya Tanzanite, Erasto Msuya kuahirishwa hadi Desemba 11, mwaka huu.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger