Home » » WAZIRI WA UCHUKUZI AFUNGUA MKUTANO WA 7

WAZIRI WA UCHUKUZI AFUNGUA MKUTANO WA 7

Written By JAK on Tuesday, October 29, 2013 | 2:29 AM



WA MAPITIO YA UTENDAJI WA SEKTA YA UCHUKUZI (JTSR 2013) UNAOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA JENGO LA GOLDEN JUBILEE (PSPF BUILDING) ,JIJINI DAR ES SALAAM TAREHE 28-29 OKTOBA 2013
 
 Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 7 wa mapitio ya utendaji wa sekta ya Uchukuzi leo asubuhi katika ukumbi wa mikutano uliopo kwenye Jengo la Golden Jubilee(PSPF BUILIDNG). Mkutano huo wa siku mbili unakutanisha wadau wa taasisi mbalimbali za sekta ya uchukuzi kujadili njia mbalimbali za kuboresha sekta ya Uchukuzi.
 
 Washiriki wa mkutano wa 7 wa Mapitio ya Utendaji wa sekta ya Uchukuzi, wakijitambulisha kabla ya mkutano huo wa siku mbili kuanza katika ukumbi wa mikutano wa Jengo la Jubilee. Mkutano huo  wa 7 unawakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya Uchukuzi kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta na kuzitafutia ufumbuzi.
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa Mkutano 7 wa mapitio ya utendaji wa Sekta ya Uchukuzi(JTSR 2013), unaofanyika katika ukumbi wa mikutano Jengo la Golden Jubilee tarehe 28-29 Oktoba 2013. Mkutano huo wa 7 unawakutanisha wadau
mbambali wa sekta ya uchukuzi kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya uchukuzi na kuzitafutia ufumbuzi ili kuboresha Uchukuzi nchini Tanzania.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Alhaj Mussa Iyombe, akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 7 wa mapitio ya utendaji wa Sekta ya Uchukuzi leo asubuhi katika ukumbi wa mikutano katika Jengo la Golden Jubilee.

Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa tatu kutoka kushoto waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi, wahisani wa Miradi ya Maendeleo na wajumbe mbalimbali waliohudhuria mkutano wa 7 wa mapitio ya utendaji wa sekta ya Uchukuzi, Unaofanyika tarehe 28-29 Oktoba katika ukumbi wa mikutano wa Jengo la Golden Jubilee. Wa kwanza kushoto waliokaa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mrs. Monica Mwamunyange, kulia kwa Waziri Mwakyembe ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka.
 
Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Usimamizi, Ufuatiliaji na Tathimini wa Wizara ya Uchukuzi , Bw. Aunyisa Meena, akiwasilisha mada kwenye mkutano wa 7 wa mapitio ya utendaji wa sekta ya
Uchukuzi, unaofanyika Tarehe 28-29 Oktoba katika ukumbi wa mikutano wa Jengo la Golden Jubilee. Mkutano huo utajadili maswala mbalimbali yanayohusu sekta ya Uchukuzi.
Habari na picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger