
Wajumbe wa Mkutano wa
15 wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya Afrika ya Kaskazini Magharibi
ya Pacif Mjini Seattle wakijiorodhesha Tayari kwa kuanza mkutano wao kwenye
Hoteli ya Red Lion Mjini Settle.

Mwana Habari wa Ofisi
ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Othman Khamis akiwa katika harakati za
dondoo za kutafuta mambo mbali mbali kwa ajili ya kutuma habari kwenye mkutano
wa Chama cha wafanyabiashara wenye asili ya Afrika Mjini Settle Nchini Marekani
alipokuwa akizungumza na mmoja wa wanajumuiya hiyo Bibi Darla Muya wa Marekani.

Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akilakiwa kwa ngoma katika mkutano wa 15
wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya Bara la Afrika wa Kaskazini
Mashariki ya Pacific unaofanyika katika Hoteli ya Kimataifa ya Red Lion kati
kati ya Mji wa Seattlle Jimbo la Washington Nchini Marekani.

Burudani katika
mkutano wa 15 wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya Bara la
Afrika wa Kaskazini Mashariki ya Pacific unaofanyika katika Hoteli ya Kimataifa
ya Red Lion kati kati ya Mji wa Seattlle Jimbo la Washington Nchini Marekani.

Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akihutubia mkutano wa 15 wa Jumuiya ya
Wafanyabiashara wenye asili ya Bara la Afrika wa Kaskazini Mashariki ya Pacific
unaofanyika katika Hoteli ya Kimataifa ya Red Lion kati kati ya Mji wa Seattlle
Jimbo la Washington Nchini Marekani.

Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiendelea kuhutubia

Wajumbe toka Zanzibar
wakibadilishana mawazo na mmoja wa wafanyabiashara waliohudhuria mkutano wa 15
wa Jumuiya ya wafanyabiashara wenye asili ya afrika Mjini Seattle.

Balozi Seif Iddi na
wajumbe wa mkutano wa 15 wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya Bara la
Afrika wa Kaskazini Mashariki ya Pacific unaofanyika katika Hoteli ya Kimataifa
ya Red Lion kati kati ya Mji wa Seattlle Jimbo la Washington Nchini Marekani.
Wa pili kulia ni Afisa Ubalozi Marekani, Bw Suleiman

Profesa Margareth Kihara Mshauri wa masuala ya wajasiri
amali Mjini Seattle akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha wafanyabiashara
wenye viwanda na wakulima Zanzibar Abdulla Abass wakati wa mapumziko wa Mkutano
wa 15 wa Jumuiya ya wafanyabiashara wenya asili ya Afrika Mjini Settle. Kati
kati yao ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na
wakulima Zanzibar bwana Ali Aboud Mzee.

Waziri wa Biashara,
Viwanda na Masoko Zanzibar aiyevaa Kipkapa na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Ali
Khalid Mirza wakibadilishana mawazo na mmoja wa wafanyabiashara waliohudhuria
mkutano wa 15 wa Jumuiya ya wafanyabiashara wenye asili ya afrika Mjini
Seattle.

Mfanyabiashara wa
chama cha wafanyabiashara kutoka Afrika
Kusini Bwana Ndaba Cyril akifurahia na
kuridhika na vipeperushi vya mambo mbali mbali ya Zanzibar kwenye meza ya
Wafanyabiashara wa Zanzibar katika maonyesho yaliyokuwa nje ya ukumbi wa
Mikutano wa Red Lion ambao ulifanyika Mkutano wa 15 wa Jumuiya ya
wafanyabiashara wenye Assili ya Afrika Mjini Seattle.

Mwenyhekiti wa chama
cha Wafanyabiashara wenye viwanda na wakulima Zanzibar Abdull Abass akimkabidhi
zawadi maalum ya Picha inayoonyesha mandhari ya Zanzibar iliyosarifiwa kwa
majani ya Gomba Mjumbe wa Baraza la Mji wa Seattle aliyemuwakilisha Meya wa Mji
huo Bw. Bruce Harrel wakati wa chakula cha mchana kwenye Mkutano wa Jumuiya ya
wafanyabiashara wenye asili ya Afrika Mjini Seattle. Picha zote na Hassan Issa
wa OMPR.
-----------------------------------
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
alisema wakati umefika kwa Bara la Afrika kuhakikisha kwamba Mataifa yaliyomo
ndani ya Bara hilo yanajikita zaidi katika
mfumo mpya wa uwekezaji badala ya ile tabia ya mataifa hayo kuendelea
kufanywa soko la bidhaa zinazotoka na kuzalishwa nje ya Bara hilo.
Balozi Seif alitoa kauli hiyo nzito kwenye mkutano wa 15 wa
Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya Bara la Afrika wa Kaskazini Mashariki
ya Pacific unaofanyika katika Hoteli ya Kimataifa ya Red Lion kati kati ya Mji
wa Seattlle Jimbo la Washington Nchini Marekani.
Alisema Bara la Afrika limebarikiwa kuwa na utajiri mkubwa
wa mali asili, rasilmali pamoja na vivutio kadhaa vya utalii ambazo vikitumika
vyema vinafursa ya kulipatia maendeleo makubwa na ya haraka bara hili
linaloendelea kukumbwa na umaskini na maradhi.
Balozi Seif alifahamisha kwamba mkazo unapaswa kuchukuliwa
na mataifa hayo katika kuona miundo mbinu ya mawasiliano, usafiri, Utalii na
hata makazi yanaimarishwa ili kuongeza nguvu za uzalishaji sambamba na
kuimarisha uchumi kwa ustawi wa jamii za Bara la Afrika.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliupongeza
Uongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya Afrika ya Mjini Mjini
Seattlle Nchini Marekani kwa mipango yake iliyojipangia ya kusaidia nguvu za
uzalishaji kwa taasisi na vyama vya wafanyabiashara vya Nchi changa wakilenga
zaidi Barani Afrika.
Balozi Seif aliwaomba wafanyabiashara wa Mji wa Seattle
kupitia jumuiya yao kufikiria kutoa upendeleo kwa Zanzibar katika kuwekeza kwa
vile Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejitahidi kuimarisha miundo mbinu
mbali mbali kwa lengo la kutoa fursa bora kwa wawekezaji kuwekeza maeneo
tofauti ya Visiwa vya Unguja na Pemba.
Alifahamisha kwamba zipo fukwe nzuri pamoja na viungo {
Spice } vinavyotoa ushawishi kwa wawekezaji wan je ya nchi kuhamasika kuwekea
vitega uchumi vya katika masuala ya Utalii.
“ Sera yetu ya uwekezaji iko wazi na inatoa fursa kwa
wawekezaji wote iwe wale wa taasisi na mashirika ya kigeni na hata wale
wazalendo kuwekeza katika maeneo tafauti hasa yale ya utalii ambayo Serikali
yetu imeyatilia mkazo zaidi katika kudaidia uchumi wake “. Alisisitiza Balozi
Seif.
Akigusia maeneo mengine kama Kilimo, Viwanda Vidogo vidogo,
mazao ya viungo pamoja na Mawasiliano, Balozi Seif alisema milango iko wazi kwa
wawekezaji wa Marekani kutumia fursa hiyo ili kusaidia uchumi wa Zanzibar
sambamba na kuongeza ajira hasa kwa kundi kubwa la Vijana wanaomaliza masomo
yao wakiwa hawana kazi za kufanya.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kupitia mkutano huo
aliipongeza Serikali ya Marekani kwa jitihada inazochukuwa za kuendelea kuiunga
mkono Zanzibar kwenye harakati zake za kujinasua kiuchumi na kujimarisha ustawi
wa Wananchi wake.
Alitolea mfano wa mradi ya kataa malaria Zanzibar
uliopunguza maradhi yazaidi ya asilimia 80% ndani ya Visiwa vya Zanzibar, mradi
wa umeme wa wats 100, ujenzi wa bara bara zenye urefu wa kilomita 35 Kisiwani
Pemba pamoja na uimarishaji wa elimu ni miongoni mwa msaada mkubwa uliotolewa
na Nchi hiyo kwa Zanzibar.
Alieleza kwamba maisha na harakati bora za kimaisha miongoni
mwa wananchi wengi wa Zanzibar imefanikiwa na kukua kutokana na miundo mbinu
iliyowekwa na Serikali kupitia washirika wa maendeleo yakiongozwa na lile la
changamoto ya millennia la Marekani { MCC }.
Naye akitoa salamu za Chama cha wafanyabiashara, wenye
viwanda na wakulima Zanzibar Mwenyekiti wa Chama hicho Nd. Abdulla Abass
aliwaeleza wajumbe wa Mkutano huo wa Jumuiya ya wafanyabiashara wwenye asili ya
Afrika kwamba sekta ya bahari Kuu
Zanzibar bado ina nafasi kubwa ya kuwekezwa na wawekezaji wa Marekani.
Nd. Abass alisema uvuvi wa Bahari kuu Zanzibar ambao unaweza
kutoa ajira kubwa kwa vijana pamoja na kuongeza mapato makubwa bado haujapata
uwekezaji katika kipindi kirefu.
Alisema utafiti unaonyesha wazi kwamba Bahari
inayovizunguuka Viziwa vya Zanzibar bado ina utajiri mkubwa wa rasilmali
inayoweza kunyanyua uchumi na mapato ya Taifa.
Mapema Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya
Afrika Bwana Gishuru Peter jumuiya hiyo ilyoanzishwa karibu miaka 16 iliyopita
katika mikakati yake ya baadaye imelenga kuvisaidia vyama na taasisi za
wafanyabiashara zipatazo 16 barani Afrika.
Bwana Gishuru alisema hatua hiyo imepangwa ili kuziongezea
nguvu jumuiya mbali mbali Barani Afrika
ziweze kujiendesha vyema kiuchumi na kustawisha jamii zinazowazunguuka.
Hata hivyo baadhi ya wataalamu waliopata fursa ya kutoa
salamu na mada kwenye mkutano huo wa 15 wa jumuiya ya wafanyabiashara wenye
asili ya Afrika ya Kaskazini Magharibi ya Pacific Mjini Seattle walisema Bara
la Afrika bado linaendelea kukumbwa na wimbi la idadi kubwa ya watu wanaozaliwa
bila ya mpango.
Mtaalamu wa masuala ya takwimu kutooa chuo Kikuu cha Seattle
Bwana Tonny Kelly alisema ukanda wa Mataifa yaliyomo ndani ya jangwa la Sahara
umekuwa ukikabiliwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu waliofikia asilimia 7.9%
hadi mwaka huu wa 2013.
Bwana Tonny alisema kiwango hicho kikubwa kinatishia ustawi
wa jamii zilizomo ndani ya ukanda huo ambacho hakiendani sambamba na ukuaji wa uchumi wa Mataifa hayo.
Mtaalamu huyo wa masuala ya takwimu alifafanua kwamba zipo
baadhi ya nchi za Afrika zinaonyesha kupata mafanikio kiasi kutokana na mpango
ulioanzishwa wa pamoja wa Kibiashara
kati ya Marekani na Afrika wa { AGOA } ambao umetoa fursa kwa wafanyabiashara
wa Mataifa kuuza bidhaa zao Nchini Marekani kwa mpango maalum wa mashirikiano
unaozingatia unafuu wa ushuru kwa bidhaa hizo.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
9/11/2013.

Post a Comment