
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi akisalimiana na Mmoja wa wanajumuiya ya Watanzania wanaoishi
Mjini Seattle,Bibie Samia Mshangama mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa Seattle kuanza ziara ya wiki moja ya Kiserikali Jimboni
humo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif akibadilishana mawazo na Afisa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania Nchini
Marekani na Canada Mama Munaka Nje ya Uwanja wa ndege wa Seattle mara baada ya
kuwasili.Kushoto ya Balozi ni Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed, na kulia ni
mkewe Mama Asha Suleiman Iddi pamoja na wana jumuia ya Watanzani wanaoishi
kwenye Mji huo Fatma Pazi na Samia Mshangama.

Mwanachama wa Jumuiya ya Watanzania
wanaoishi Seattle Ubwa Jaha akimfariji Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif kwa uchovu wa safari wakati alipowasili Mjini Seattle kuanza ziara
ya wiki moja.
Kulia ya Balozi ni Afisa Utawala wa
Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani Mama Munaka na kushoto yake ni Mkewe Mama
Asha Suleiman Iddi.

Mkurugenzi wa Kituo cha Inter Connection
cha clabu ya Rotary Mjini Seattle Bwana Charles Brennick akitoa ahadi Mbele ya
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na ujumbe wake walipotembelea
kituo hicho ya kusaidia kompyuta kwa ajili ya Skuli za Zanzibar.Kushoto ya Bwana Charles ni Waziri wa
Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazrui.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanziar Balozi
Seif Ali Iddi akiuongoza mkutano wa dharura na wajumbe aliofuatana nao wa
kupanga mikakati ya ziara yake ya wiki moja Mjini Seattle Nchini Marekani
uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Marriot Mjini Seattle.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Post a Comment