Home » » Kung’olewa kwa Zitto, Mkumbo: Chadema mikoani watofautiana

Kung’olewa kwa Zitto, Mkumbo: Chadema mikoani watofautiana

Written By JAK on Sunday, November 24, 2013 | 10:25 PM

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhVZGg7lGlBeFkYWWovLeaRLGiCeRIQ23YFOYZ5nSzl7Nwh1DvAZ_HtC72gbcMz6mIN_7i55yFchjSrXBI0UNDyxVbK4Y04Q-EG-yGh8fvOtXgMPrTNxdJlws4mFyW4NcPhatTw7e6c6Kc/s1600/Kamanda+Makelele,+Katibu+mwenezi+wa+moshi+mjini+aki+wapa+nasaha+viongozi+wa+Chadema+UK.JPG

Na Waandishi Wetu, Mwananchi

Kwa ufupi
Vikao vya faragha Singida, Rukwa, Arusha, Kigoma na Mwanza vinaonyesha tofauti za kitaratibu na pengine kiitikadi kati ya wanachama wa ngazi za chini na wale wanaowaongoza, huku baadhi wakilaani maamuzi ya Chadema kuwavua uongozi Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo, wakati wengine wakiyachukulia kama hatua ya msingi katika kukuza demokrasia.

Wanachama wa Chadema mikoa mbalimbali nchini pamoja na wananchi wametoa maoni tofauti kuhusu uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho wa juzi kuwavua uongozi viongozi wake watatu; Naibu Katibu Mkuu wake Zitto Kabwe na Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo na mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.

Singida

Kutoka mkoani Singida, uongozi wa chama hicho  jana ulifanya kikao cha faragha kujadili uamuzi wa chama hicho, huku baadhi ya wananchi wakiuelezea uamuzi  huo kuwa umetokana na pupa na kushindwa kuvumiliana, wengine wakitishia kujitoa katika chama hicho.

Kwa zaidi za saa 5 uongozi huo ulikuwa ukijadili hatua hiyo huku ukiahidi kutoa taarifa yake baada ya kikao hicho kilichokuwa kikiendelea hadi baada ya saa 7 mchana.

Habari zaidi kutoka Wilaya ya Iramba mkoani humo zinasema kuwa wanachama wa Chadema wilayani humo wametishia kurudisha kadi za chama hicho kilichokuwa kimeanza kujizolea umaarufu wakisema watafanya hivyo ikiwa Chadema ‘watalitosa jembe’ lao.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili walisema kuwa hatua hiyo inaweza kuipunguzia umaarufu Chadema na kwamba ustawi wa vyama vingi vya siasa unaponzwa na pupa, jazba hata kukosa uvumilivu.

“Kikundi hiki cha viongozi kinasababisha Chadema kumeguka kama tulivyosikia juzi. Kwa maoni yangu kabla hakijawavua uongozi Zitto, Dk Mkumbo na Mwigamba, kilikuwa kinashabikiwa na asilimia 90, hapa Singida, lakini baada ya tukio la juzi la kuwavua uongozi baadhi ya viongozi, nina hakika kinashabikiwa na asilimia 30 ya wananchi,” alisema Juma Mdida.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TLP Wilaya ya Singida, Athumani Nkii, alisema kuwa ustawi  wa vyama vingi vya siasa unaponzwa na vitendo vya pupa, jazba na ubinafsi wa baadhi ya viongozi wake baada ya majina yao kupata umaarufu,wakisahau kuwa umaarufu huo unachangiwa na chama husika.

“Kwa upande wa Kabwe Zitto, nadhani safari zake za nje ya nchi na suala la mapesa ya Uswisi, zitakuwa hazina baraka za Chadema. Kuhusu Dk Kitila Mkumbo, sina kabisa fununu ya madhambi yake,”alisema.

Rukwa

Barua ya kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti Chadema Tanzania Bara, Said Amour Arfi ambaye pia ni Mbunge wa Mpanda imesambazwa  kwa wapiga kura wake na wananchi wa jimbo hilo ili  wafahamu sababu za msingi za yeye kujiondoa katika nafasi yake.

Katibu wa mbunge huyo, Joseph Mona, alipata taarifa za uamuzi huo wa ghafla, aliosema kuwa ni sahihi.Wanachama wa Chadema mikoa mbalimbali nchini pamoja na wananchi wametoa maoni tofauti kuhusu uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho wa juzi kuwavua uongozi viongozi wake watatu; Naibu Katibu Mkuu wake Zitto Kabwe na Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo na mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.

Singida

Kutoka mkoani Singida, uongozi wa chama hicho  jana ulifanya kikao cha faragha kujadili uamuzi wa chama hicho, huku baadhi ya wananchi wakiuelezea uamuzi  huo kuwa umetokana na pupa na kushindwa kuvumiliana, wengine wakitishia kujitoa katika chama hicho.

Kwa zaidi za saa 5 uongozi huo ulikuwa ukijadili hatua hiyo huku ukiahidi kutoa taarifa yake baada ya kikao hicho kilichokuwa kikiendelea hadi baada ya saa 7 mchana.

Habari zaidi kutoka Wilaya ya Iramba mkoani humo zinasema kuwa wanachama wa Chadema wilayani humo wametishia kurudisha kadi za chama hicho kilichokuwa kimeanza kujizolea umaarufu wakisema watafanya hivyo ikiwa Chadema ‘watalitosa jembe’ lao.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili walisema kuwa hatua hiyo inaweza kuipunguzia umaarufu Chadema na kwamba ustawi wa vyama vingi vya siasa unaponzwa na pupa, jazba hata kukosa uvumilivu.

“Kikundi hiki cha viongozi kinasababisha Chadema kumeguka kama tulivyosikia juzi. Kwa maoni yangu kabla hakijawavua uongozi Zitto, Dk Mkumbo na Mwigamba, kilikuwa kinashabikiwa na asilimia 90, hapa Singida, lakini baada ya tukio la juzi la kuwavua uongozi baadhi ya viongozi, nina hakika kinashabikiwa na asilimia 30 ya wananchi,” alisema Juma Mdida.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TLP Wilaya ya Singida, Athumani Nkii, alisema kuwa ustawi  wa vyama vingi vya siasa unaponzwa na vitendo vya pupa, jazba na ubinafsi wa baadhi ya viongozi wake baada ya majina yao kupata umaarufu,wakisahau kuwa umaarufu huo unachangiwa na chama husika.

“Kwa upande wa Kabwe Zitto, nadhani safari zake za nje ya nchi na suala la mapesa ya Uswisi, zitakuwa hazina baraka za Chadema. Kuhusu Dk Kitila Mkumbo, sina kabisa fununu ya madhambi yake,”alisema.

Rukwa

Barua ya kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti Chadema Tanzania Bara, Said Amour Arfi ambaye pia ni Mbunge wa Mpanda imesambazwa  kwa wapiga kura wake na wananchi wa jimbo hilo ili  wafahamu sababu za msingi za yeye kujiondoa katika nafasi yake.

Katibu wa mbunge huyo, Joseph Mona, alipata taarifa za uamuzi huo wa ghafla, aliosema kuwa ni sahihi.

Naye Katibu Mwenezi wa Chadema Mkoa wa Rukwa, John Matongo alisema kuwa kilichotokea ni msukosuko jambo ambalo ni kitu cha kawaida kwenye vyama vya siasa.

“Hata gari linapokuwa katika safari huwa linakumbana na matatizo mbalimbali kabla ya kufika mwisho wa safari, hivyo kikubwa kwao ni kukaa meza moja ya mazungumzo,” alisema Matongo.

Naye Erasto Jetha mkazi wa Mpanda alipongeza uamuzi wa Arfi akieleza kwa  muda mrefu wamekuwa wakipuuzwa wanapotoa ushauri kuhusu kukiimarisha chama hicho.

Joseph Makumbule  anasema kuwa Arfi ameonyesha uzalendo kwa kujiuzulu kwake hasa kwa wananchi wa Katavi.

Kigoma

Kutoka mkoani Kigoma, wakazi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini wametaka Zitto arejeshewe nafasi zake wakihofia mpasuko katika chama hicho.

Mmoja wa wakazi hao, Abdi Mtemi wa Kijiji cha Msiba alisema: “Zitto arudishiwe nafasi yake ya unaibu katibu mkuu, nina hofu kuwa chama kitapasuka.”

Naye Shabani Musa wa Kijiji cha Kigaza alisema kuwa chama ni zaidi ya mtu na kwamba anapongeza uamuzi wa Chadema huku akiungwa mkono na Atanas John wa Kamara aliyeeleza kuwa chama ndicho kinaamua, hivyo lazima viongozi waheshimu mamlaka .

Arusha

Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha(Chadema), Joshua Nassari amesema kuwa anamsikitikia Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe kwa kuvuliwa nyadhifa, lakini akamtaka kujipanga upya akieleza kuwa bado ana nafasi ya kung’ara kwenye siasa za Tanzania akiwa Chadema.

Nassari alisema kuwa kilichomtokea Zitto ni jambo la kawaida katika siasa na bado anaweza kujipanga ndani ya Chadema na kufikia malengo yake. “Tukio hili linatupa funzo kuwa hakuna mwenye uwezo zaidi ya chama kwani ndicho kimemfikisha alipo, lakini naamini Zitto ana uwezo wa kukiri makosa na kujipanga upya kwani bado ni kijana na bado ana nafasi ya kujipanga,”alisema Nassari.

Alisema kuwa binafsi aliingia kwenye siasa kutokana na kuvutiwa na Zitto tangu akiwa  Chuo Kikuu na anaamini kwamba safari ya Zitto haitaisha baada ya kuvuliwa uongozi.Akizungumzia sababu za kuvuliwa nafasi za uongozi, Nassari alisema kuwa ni sahihi akieleza kuwa haiwezekani  kufuga nyoka mwenye sumu ndani ya nyumba.

“Ni bora uwe nyikani ukijua kuna simba zaidi ya 10 kuliko kuwa ndani ya nyumba na nyoka mwenye sumu,” alisema Nassari.

Mwanza

Kutoka mkoani Mwanza habari zinaeleza kuwa  chama hicho katika Manispaa ya Bukoba Mjini kimepongeza uamuzi  wa kuwavua nyadhifa zao viongozi hao wa ngazi za juu na kusema uamuzi huo  unapaswa kuwa fundisho kwa viongozi wengine.

Kwa mujibu wa tamko hilo lililosainiwa na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Bukoba Mjini, Victor Sherejey na Katibu Mwenezi, Peter Mweyunge,  chama ni muhimu kuliko kiongozi na kwamba kila kiongozi anapaswa kuheshimu chama kupitia Katiba na siyo kuwa juu ya chama.

Tamko hilo lilifafanua kwamba hatua hiyo inapaswa kuigwa na vyama vingine vyenye tabia ya kuwalinda viongozi wake waovu.

Habari imeandaliwa na Gasper Andrew, Singida; Mussa Juma, Arusha;  Frederick Katulanda, Mwanza; Anthony Kayanda, Kigoma na  Mussa Mwangoka, Rukwa.
Share this article :

Post a Comment

Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger