Home » » Mil. 53/- zatolewa kwa vikundi vya uzalishaji mali

Mil. 53/- zatolewa kwa vikundi vya uzalishaji mali

Written By JAK on Sunday, November 24, 2013 | 6:15 PM

 http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2012/10/IMG_3959.jpg
Moshi Chang’a

By Peti Siyame, Kalambo (Habari Leo)

SERIKALI imetoa mikopo ya zaidi ya Sh milioni 53.3 kwa vikundi vya uzalishaji mali 18 katika Halmashauri ya wilayani Kalambo mkoani Rukwa katika kipindi cha mwaka 2012/13.

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Moshi Chang’a amebainisha hayo wakati wa mahojiano maalumu na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni yaliyofanyika katika mji mdogo wa Matai wilayani humo.

Aliongeza kuwa hatua hiyo ya Serikali kutoa kiasi hicho cha fedha, ikiwa ni katika kutekeleza Sera za Taifa ya maendeleo ya wanawake na jinsia ya mwaka 2000/ 03 na Sera ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi ya 2004.

“Halmashauri ya Wilaya hii ya Kalambo ina vikundi vya uzalishaji mali 28 kati ya hivyo vikundi 18 vilipata mkopo kutoka Serikalini wa Kiasi cha Sh 53,384,000- kwa mwaka wa fedha uliopita,” alibainisha.

Alifafanua kuwa mikopo hiyo ilitolewa kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake na Maendeleo ya Vijana pamoja na Mfuko wa kuendeleza Bonde la Ziwa Tanganyika – Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger