Home » » Ngugi atunukiwa ‘Udokta wa Fasihi' UDSM

Ngugi atunukiwa ‘Udokta wa Fasihi' UDSM

Written By JAK on Sunday, November 24, 2013 | 10:37 PM


Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Balozi Nicholaus Kuhanga (Kushoto) akimtunuku Shahada ya Heshima ya Udaktari Mtunzi wa Vitabu vya Kiafrika, Profesa Ngugi wa Thiong’o kwenye Mahafali ya 43 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam jana. PICHA | VENANCE NESTORY
Na Goodluck Eliona, Mwananchi

Kwa ufupi
    Profesa Ngugi wa Thiong’o ambaye ni nguli wa fasihi za lugha na pia ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha California huko Marekani, alitunukiwa shahada hiyo jana, Dar es Salaam wakati wa Mahafali ya 43 ya UDSM.


Dar es Salaam. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kimemtunuku Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Fasihi ya Lugha, Profesa Ngugi wa Thiong’o kutokana na mchango wake mkubwa kwa Bara la Afrika katika kujikomboa kiakili dhidi ya ubeberu wa lugha za kigeni.

Ngugi ambaye ni nguli wa fasihi za lugha na pia ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha California huko Marekani, alitunukiwa shahada hiyo jana, Dar es Salaam wakati wa Mahafali ya 43 ya UDSM.

Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa Rwekaza Mukandala, alisema chuo kimeamua kumpa shahada hiyo kutokana na mchango wake wa kupinga chuki na dharau zinazofanywa na mataifa ya Ulaya dhidi ya lugha za Afrika.

“Katika jitihada hizo, Chuo Kikuu kimeruhusu tasnifu (Thesis) za Shahada ya Uzamili na Uzamivu katika Kiswahili ziwasilishwe katika Lugha ya Kiswahili. Pia Chuo kinasisitiza kuwa tasnifu zote hapa chuoni ziwe na muhtasari mfupi ulioandikwa kwa Kiswahili,” alisema.

Akishukuru baada ya kukabidhiwa shahada hiyo , Ngugi alisema hiyo ni shahada yake ya nane kutunukiwa na vyuo mbalimbali duniani na ya pili kwa  Afrika.   
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger