Rais Jakaya Kikwete (katikati) akibadilishana mawazo na
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (kushoto)
nyumbani kwa marehemu Dkt. Sengondo Mvungi walipokwenda kuipa pole familia.
Kulia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia na Mjumbe wa Tume Waziri Mkuu
Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph
Warioba akitia saini kitabu cha maombelezo ya kifo cha Mjumbe wa Tume hiyo Dkt.
Sengondo Mvungi nyumbani kwake Kibamba jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Richard Lyimo akimpa
pole mke wa marehemu Dkt. Sengondo Mvungi, Bi. Anna Mvungi wakati Wajumbe wa
Tume walipokwenda kumpa pole.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph
Warioba wakifurahia jambo na Waziri wa Katiba na Sheria Mathias Chikawe
(kushoto), Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na
Mjumbe wa Tume Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim (kulia) walipokutana
nyumbani kwa marehemu Dkt. Sengondo Mvungi Kibamba jijini Dar es Salaam. (Picha
na Tume ya Katiba).
Tume ya Mabadiliko ya Katiba inawafahamisha wananchi kuwa
taratibu za
kuusafirisha mwili wa Mjumbe wake, Dkt. Sengondo Mvungi
aliyefariki
nchini Afrika Kusini zimekamilika na mwili wake unatarajia
kuwasili
nchini siku ya Ijumaa, Novemba 15, 2013.
Baada ya kuwasili, mwili huo utahifadhiwa katika Hospitali
ya Jeshi Lugalo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Aidha,siku ya Jumamosi, Novemba 16, 2013 kutafanyika Ibada ya
mazishi katika
Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam
kuanzia saa
4:00 asubuhi. Baada ya misa, marehemu ataagwa katika Viwanja
vya
Karimjee kuanzia saa 6:30 mchana siku hiyohiyo ya Jumamosi,
Novemba 16,2013.
Aidha,Marehemu Dkt. Mvungi anatarajiwa kusafirishwa siku ya
Jumapili, Novemba
17, 2013 kwenda Kisangara Juu, Wilaya ya Mwanga mkoani
Kilimanjaro kwa
ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu,
Novemba 18,2013.
Dkt.Mvungi alifariki jana (Jumanne, Novemba 12, 2013) katika
Hospitali ya
Millpark jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini
alikopelekwa kwa ajili
ya uchunguzi na matibabu zaidi akitokea Kitengo cha Mifupa
Muhimbili
(MOI) aliokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake
Kibamba, wilaya
ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi
vibaya kichwani
usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, Novemba 3, 2013.
Wakati huohuo, Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
wakiongozwa na
Mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba leo (Jumatano, Novemba
13, 2013)
wameungana na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete kufika nyumbani kwa marehemu Dkt.
Mvungi eneo la
Kibamba jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa pole kwa
familia, ndugu
na jamaa wa marehemu Dkt. Mvungi.

Post a Comment