Mwenyekiti wa kamati ya usajili Abdallah
Binklebu amesema leo jijini Dar es salaam kuwa wamefikia uamuzi huo
baada ya kupokea maoni ya wachezaji mbali
mbali wa zamani kuhusu kiwango cha timu.
"Tumempa notisi ya siku 30 ili tuendelee
kutafuta kocha mwingine, na tupo kwenye
mchakato wa kumlipa stahiki zake,
tuachane kwa amani.
“Mwanzoni alipandisha kiwango cha timu, kilipanda sana, lakini baadaye kiwango kikaanza kushuka, tukasema tumpe muda kidogo, lakini tunaona mambo yanazidi kuharibika, hivyo tumeamua kuachana naye kwa sababu hana jipya, sisi tunalenga michuano ya kimataifa zaidi sasa kwa kiwango hichi hatutafika mbali ni lazima tuchukue hatua za haraka zaidi,”alisema.
Kuhusu Wajumbe wengine wa benchi la Ufundi, Bin Kleb alisema kwamba taratibu nyingine zinafuata na ndani ya wiki hii kuna maamuzi mengi makubwa ambayo klabu yake itayafanya.
Hata hivyo tayari Brandts alikabidhiwa
barua yake ya kusitishiwa mkataba rasmi
juzi na jana baada ya mazoezi Makamu
Mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga
alikutana na wachezaji na kuzungumza nao
kwa zaidi ya nusu saa.
Kocha Brandts amesema kwa kifupi "Nasubiri notisi ya siku 30 imalizike. Kuna kitu nitaongea lakini sio sasa. Sasa hivi msikilizeni Abdallah (Binkleb) anachosema ukifika muda na mimi nitazungumza."
Post a Comment