Home » » NSSF YACHANGIA MILIONI 100 MFUKO WA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI ZANZIBAR

NSSF YACHANGIA MILIONI 100 MFUKO WA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI ZANZIBAR

Written By JAK on Tuesday, December 24, 2013 | 1:53 AM


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar (SMZ), Dk. Mohamed Shein akimkabidhi tuzo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Chiku Matesa kutokana na kutambua mchango wa shirika hilo wa kuchangia sh. milioni 100 wakati wa uzinduzi wa Mfuko wa Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi Zanzibar, uliokwenda sambamba na harambee ya kuchangia mfuko huo. Hafla hiyo ilifanyika mjini Zanzibar, mwishoni mwa wiki. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Chiku Matesa (kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (wa tatu kushoto), Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu (wa pili kushoto) wakiwa na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (kulia), Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu (katikati), wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Mfuko wa Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi Zanzibar, iliyokwenda sambamba na harambee ya kuchangia mfuko huo. 
Rais Dk, Shein akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mashirika na Taasisi mbalimbali zilizochangia Mfuko wa Uwezeshaji Zanzibar.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger