Home » » BENKI YA FBME ARUSHA YAKABIDHI MISAADA KWA WATOTO YATIMA

BENKI YA FBME ARUSHA YAKABIDHI MISAADA KWA WATOTO YATIMA

Written By JAK on Monday, December 30, 2013 | 7:00 AM


DSCF1996Meneja wa benki ya FBME  Tawi la Arusha Ramadhani Lesso  akikabidhi misaada mbalimbali kwa mratibu wa kituo cha Samaritan Village  Josephat Mmanyi kilichopo Moshono kwaajili ya sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya,misaada hiyo iligharimu kiasi cha shilingi Laki saba na nusu,kwa vituo viwili pamoja na kituo cha Abu-Abdulrahamani kilichopo  jijini Arusha.
DSCF2008Meneja wa benki ya FBME  Tawi laArusha Ramadhani Lesso  akikabidhi misaada mbalimbali kwa Aziza Suleman ambaye ni  dada mlezi wa kituo cha Abu-Abdulrahamani kilichopo Jr  jijini  jijini hapa kwaajili ya sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya,
Na Pamela Mollel,Arusha
Mamlaka zinazohusika na utowaji wa vibali vya kumuliki vituo vya watoto yatima hapa Nchini vimetakiwa kuwa makini na kufwatilia mwenendo mzima wa vituo hivyo kwa kuwa baadhi ya wamiliki wamekuwa sio wahaminifu kwa watoto hao.Pia Jamii imehaswa kutokufumbia macho utapeli huo na badala yake kuwafichua ili wachukuliwe hatua kali za kisheria
Rai hiyo imetolewa na Meneja wa benki ya FBME  Tawi laArusha Ramadhani Lesso wakati akikabidhi misaada mbalimbali kwa vituo viwili vya watoto yatima jijini hapa kwa ajili ya sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya
Lesso alisema kuwa vipo vituo vya watoto yatima ambavyo vimekuwa vikikiuka utaratibu na kuamua kujiingiza katika utapeli wa kujinufaisha kupitia mgongo wa watoto yatima.Alisema kuwa ni vyema Mamlaka zinazohusika kufwatilia kwa ukaribu vituo vya watoto yatima kwa kuwa baadhi ya wamiliki wamejiingiza katika utapeli hivyo kuwadhulumu yatima haki yao
Pia aliwataka jamii kushiriki kuwafichua wamiliki wa vituo ambao wamekuwa wakienda kinyume na utararibu ili wachukuliwe hatua kali za kisheria ,“Ni dhambi kubwa kwa wale wanaofanya biashara ya hii ya kuwadhulumu watoto yatima,,,Zipo njia za kujipatia fedha lakini siyo kwa njia ya utapeli wa namna hii”alisema Lesso.
Vituo vilivyopatiwa msaada na benki hiyo ni pamoja na kituo cha Abu-Abdulrahamani kilichopo Jr,Samaritan Village kilichopo Moshono jijini hapa,vifaa vyote viligharimu kiasi cha shilingi Laki saba na nusu
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger