Na Geofrey Tengeneza
Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania-JWTZ Jenerali mstaafu George
Waitara ameihakikishia Bodi ya Utalii Tanzania –TTB kuwa Jeshi hilo litaendelea kuunga juhudi
za TTB katika kuvitangaza vivuto vya Utalii vya Tanzania ukiwemo mlima Kilimanjaro kupitia
msafara wa kupanda mlima Kilimanjaro maarufu kwa jina la Uhuru Expedition unaofanywa na
Jeshi la Wananchi kila mwaka katika kuadhimisha Uhuru wa Tanzania.
Jenerali Waitara ambaye ndiye Kiongozi na msimamizi mkuu wa Uhuru Expedtion aliyasema
hayo jana wakati akiwapokea wapanda mlima walioshiriki katika msafara huo mwaka huu
ulioratibiwa na kufadhiliwa na Bodi ya Utalii Tanzania katika eneo la Hifadhi ya Taifa ya
Kilimanjaro –KINAPA Marangu Moshi.
“Tunaishukuru sana Bodi ya Utalii kwa kushirikiana nasi
kwa mara nyingine tene katika msafra huu, lakini pia nawashukuru sana KINAPA kwa msaada
wote waliotupa na niwahakikishie kuwa Jeshi litaendelea kuutangaza utalii wetu wa Tanzania
ukiwemo utalii wa kupanda mlima Kilimnjaro” alisema Jenerali msataafu Waitara ambaye pia
aliwakabidhi vyeti wapanda mlima sita.
Mapema Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTB Balozi Charles Sanga ambaye pia
alikuwa miongoni mwa wapanda mlima alisema kuwa Bodi ya Utalii inafurahi kuona kuwa Uhuru
Expedition iliyoasisiwa na Jeshi la wananchi wa Tanzania inaendelea kuimarika na kutekeleza
malengo ya kuanzishwa kwake na kwamba kwa kutambua mchango wa Expedition hii ndiyo
maana TTB imekuwa ikiiunga mkono. Amemsifia Jenerali Waitara kwa kuisimamia vema
Expediton hii na kwa juhudi zake za kuhakikisha kila mwaka tukio la kupanda mlima la Uhuru
Expedition linafanyika.
Naye Kiongozi wa Msafara uliopanda mlima mwaka huu Meja Jenerali Christopher Gimongi
amesema msafara huu uliokuwa na wapanda mlima saba ulianza kupanda mlima tarehe 6/12/
2013 kupitia njia ya Marangu na kwamba ni wapanda mlima watatu tu akiwemo yeye walioweza
kufika kileleni. Meja Jenerali Gimongi alisisitiza umuhimu wa Wizara ya Maliasili na Utalii
kufadhili Uhuru Expedition kama alivyoahidi Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Balozi Khamis
Kagasheki wakati wa tukio kama hilo kama mwaka jana.
Tukio la kupanda mlima mwaka huu kupitia Uhuru Expedition lilishirikisha wafanyakazi wawili
wa TTB, Mwenyekiti wa TTB baolzi Charles Sanga, Meja Jenerali Mstaafu Christopher
Giomongi na wafanyakazi watatu kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa akiwemo
mwanamke mmoja.
Mkuu wa JWTZ msataafu Jenerali George Waitara (kulia) akimtunuku Mwenyekiti wa TTB
Balozi Charles Sanga cheti baada ya kushiriki kupanda mlima Kilimanjarao katika kuadhimisha
miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Anayeshuduia kushoto ni Mhifadhi Mkuu wa KINAPA
Bwana Erastus Lufungulo
Jenerali Waitara (kulia) akimtunuku cheti Meja Jenerali Christopher Gimongi ambaye alikuwa
kiongozi wa msafara wa wapanda mlima wa ‘Uhuru Expedition’ mua mfupi baada ya wapanda
mlima hao kukamilisha zoezi hilo hapo jana.
Wapanda mlima kutoka TTB, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakiwa katika picha
ya pamoja na mgeni rasmi Jenerali mstaafu George Waitara (mwenye jaketi jeupe), waongoza
wapanda mlima, na Mkuu wa Hifadhi ya KINAPA muda mfupi baada ya kukabidhiwa vyeti.
Post a Comment