Home » » VIJANA WASOMI MKOA WA DODOMA WAPATIWA MASHAMBA

VIJANA WASOMI MKOA WA DODOMA WAPATIWA MASHAMBA

Written By JAK on Thursday, December 12, 2013 | 4:02 AM


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr Rehema Nchimbi akisisitiza jambo alipo kuwa akiongea na Uongozi wa ngazi mbali mbali za Mkoa na baadhi ya vijana wa mkoa wa Dodoma waliokabidhiwa heka 50 za mashamba ya ushirika.
Mkuu wa Mkuu wa Dodoma Dr Rehema Nchimbi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Bibi Rechal Chuwa, Mkuu wa Wilaya ya Bahi Betty Mkwasa na Mkuu wa Magereza Wilaya ya Bahi Bw; Ramadhani H. Mabere wakiwa wameshika zana zao za kazi tayari kusaidiana na vijana zaidi ya 100 kusafisha shamba lenye heka 50 la vijana hao.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr Rehema Nchimbi akimsikiliza kwa Makini alie kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Bahi Bw Sustenance Mpandu alipo amua kuachana rasmi na Chama chake na kuungana na vijana wapenda maendeleo wa Mkoa wa Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr Rehema Nchimbi alie vaa sare ya timu ya Taifa katikati na kulia kwakwe ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Betty C. Mkwasa wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa mbali mbali pamoja na baadhi ya vijana wapenda maendeleo wa Mkoa wa Dodoma wakiinua zana zao za kilimo juu kuashiria kuwa Uhuru ni Kazi. Habari & picha na Madau Sixmund J. Begashe

Vijana nchini wametakiwa kuacha tabia ya kutumika na kutumia nguvu na akili zao kwa manufaa ya wachache bali wazitumie kwa manufaa yao na ya Taifa kwa ujumla kama ishara sahihi ya ukombozi wa vijana kifikra na kutambua kuwa Uhuru ni Kazi.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr Rehema Nchimbi katika maadhimisho ya aina yake ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania kimkoa yaliyo fanyika wilayani Bahi, Dr Nchimbi aliwapongeza vijana hao zaidi ya mia moja walio jikomboa kifikra kutoka vyuo vikuu, wahitimu na waendesha Boda Boda wa Mkoani hapa kwa kufanya maamuzi ya busara na kuondokana na fikra potofu za ajira bora ni ile ya kuajiriwa.

Dr Nchimbi alisisitiza kuwa vijana sasa waachane na Maandamano yenye sura ya uvunjifu wa amani bali maandamano hayo yawe ni yakuelekeza nguvu zao katika kujiajiri wenyewe kama walivyo fanya vijana wa Mkoa wa Dodoma kwa kuadhimisha Miaka 52 ya Uhuru wao kwa kujiweka huru kifikra na kujitafutia fursa za kimaendeleo.

Kama kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inavyo sema Vijana ni Nguvu ya Saraslimali watu Tuwaamini na Tuitumie kwa Manufaa ya Taifa letu, Dr Rehema Nchimbi ameziagiza Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma kushirikiana na vijana wote watakao kuwa huru kifikra na kujitambua kuwa wao ni raslimali muhimu ya Taifa letu.

Katika sherehe hizo zilizo pambwa na Mapanga, Nyengo na vifaa mbali mbali vya kilimo, mmoja wa kati ya viongozi wa Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wilaya ya Bahi ambae ni mwanachuo katika chuo kikuu kimoja wapo Bw Sustenance Mpandu, aliungana na vijana wenzake baada ya kukiri kwamba amekuwa huru kifikra na hivyo kuachana na utamaduni wa kupotosha kila kweli, Utamaduni ambao ulimfubaza kifira na hivyo kushindwa kuona fursa nyingi ambazo vijana wanaweza kuzitumia kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Bw Mpandu alisema kuwa yeye ni mmoja wa watu walio kuwa mstari wa mbele katika kupinga ukweli na kujitahidi kuufanya uongo uwe ukweli masikioni mwa watanzania, lakini sasa ameona alicho kuwa akikifanya ni dhambi kubwa na hakina tija kwa maslai ya Taifa hili.

Alie kuwa kiongozi huyo wa CHADEMA alitoa wito kwa vijana wote na wasomi wote nchini kuachana na dhambi ya kupotosha Ukweli kwa ajili ya maslahi ya wachache bali waungane na Serikali katika kuwaletea wanachi maendeleo na si kuikosoa serikali kila kukicha huku wakijua ukweli kuwa serikali imejitahidi sana kuwaletea wananchi wao maendeleo ndani ya miaka hii 52 ya Uhuru wetu.

Mkuu wa Wilaya ya Bahi Betty Mkwasa licha ya kuwapongeza vijana hao kwa kujikomboa kifikra aliwaahidi kuendelea kushirikiana nao ili kuhakikisha wanafikia malengo yao, pia aliwashauri kufanya kazi kwa bidii ili mafanikio watakayo yapata kutoka kwenye mashamba hayo yaweze kutoa fursa kwa vijana wengine hususani ya kuwaajiri.

Kwa niaba ya Vijana hao walio jikomboa kifikra Bw.Anyelwisye Jonas Aliupongeza uongozi wa Mkoa wa Dodoma kwa kuungana nao bega kwa bega katika safari yao hiyo ya ukombozi wa kifikra na kuhaidi kuwa watakuwa mabalozi kwa vijana wengine wenye mitazamo finyu ya kusubiri ajira ya Serikali na penginepo badala ya kujiajiri na wao kuwa waajiri wa wengine.

Katika maadhimisho hayo, Viongozi mbali mbali wa Mkoa na Wilaya walijitole pasa za kusafisha heka zote 50 na Mkururugenzi wa Halmashauri ya Wilaya kupitia Mkurugenzi wake Bi Rechal Chuwa kuahidi kuwajengea mahali atakaae kaa mtu atakae ajiriwa na vijana hao kwa ajili ya uangalizi wa shamba litakalo kuwa na mazao na mifugo.

Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger