Home » » Kampuni ya vilainishi ya Orion yaingia ubia na kampuni ya vilainishi ya Chevron kusambaza bidhaa zao

Kampuni ya vilainishi ya Orion yaingia ubia na kampuni ya vilainishi ya Chevron kusambaza bidhaa zao

Written By JAK on Thursday, December 12, 2013 | 4:28 AM


Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akizunumza na wagwni waalikwa(hawapo pichani) wakati wa hafla ya kuchaguliwa kwa kampuni hiyo kuwa wasambazaji wa Oil za Caltex nchini Tanzania.Hafla hiyo ilifanyika DAR ES Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Orion Lublicants, Beny Maregesi akizunumza na wageni waalikwa(hawapo pichani) wakati wa hafla ya kuchaguliwa kwa kampuni hiyo kuwa wasambazaji wa Oil za Caltex nchini Tanzania.Hafla hiyo ilifanyika DAR ES Salaam .

Kampuni ya vilainishi Orion, hivi karibuni waliingia ubia wa kusambaza bidhaa za wamiliki na watengenezaji wa vilainisha injini Chevron. Kampuni za vilainishi Texaco na Caltex ni miongoni mwa makampuni yanayoongoza kwenye kwenye teknolojia ya mafuta duniani. Makubaliano haya yanaifanya kampuni ya vilainishi ya Orion kuwa msambazaji pekee wa vilainisho vya Chevron kwa bidhaa yake Caltex.

Vilanishi vya Chevron kupitia Orion ina mpango wa kukuwa na kurudisha heshima yao ya kuongoza katika utoaji wa vilainisho bora. Kampuni ya Orion kwa sasa ndio kampuni pekee yenye mamlaka ya kusambaza bidhaa za Caltex pamoja na bidhaa maarufu za Delo and Havoline, vile vile Orion watatoa huduma za vilainisho viwandani na majini.

Tamko hilo lilitolewa kwenye chakula cha usiku kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ukiuzuliwa na mtendaji mkuu wa kampuni ya Orion Maregesi Manyama, meneja biashara Clint, Nickall,na wadau wengine kwenye tathiniya hii.

“Soko la Tanzania limekuwa kwa kiasi kikubwa na tumegundua kuna hitaji ya vilainishi halisi na huduma bora alisema Maregesi Manyama wa Orion”.  “Vilainishi vya Caltex vimerudi tena Tanzania na muda muafaka baada ya ripoti TBS ya hivi karibuni kuonyesha kwamba asilimia tisini ya vilainisho nchini havina ubora. Tunatazamia kuwa na mahusiano ya mda mrefu na kampuni ya vilainishi ya Chevron, kwani watatupa misingi ya ufahamu kuhusiana na vilainisho bora na kuifanya bidhaa ya Caltex kuwa chaguo la watanzania”.

“Tunashukuru kwa ushurikiano huu na kampuni ya vilainishi ya Orion na kupanua wigo wetu kutoa vilainishi bora barani Afrika.” Aliongeza Clint Nickall wa kampuni ya vilanishi ya Chevron.

Bwana Nickall aliendelea kwa kusema “Katika uchaguzi wao wa kumpata mshirika ambae atawasambazia bidhaa zao kampuni ya Chevron walikuwa makini na kuwa na imani na kampuni ya vilainishi ya Orion itaweza kuwapatia wateja vilainishi na huduma bora”.

Kampuni ya Vilainishi ya Orion yenye makao yake jijini Dar es salaam, Tanzania. ofisi zao zipo Mandela Road Buguruni. Orion wamechaguliwa kuwa wasambazaji wa kampuni ya vimiminika ya Caltex ambayo itajumuisha bidhaa za Delo Havoline. 

Mtendaji mkuu wa Orion Maregesi Manyama ni kiongozi mwenye uzoefu mkubwa kwenye nishati na ameshika nyazfa mbalimbali ndani na makampuni ya mafuta ya kimataifa. Bodi ya vilainishi ya kampuni ya Orion inaundwa na watu wanaojua vizuri vilainishi. Kampuni ya vilainishi ya Orion 

Kwa maelezo zaidi kuhusu Orion na wakurugenzi wake tembelea tovuti ya www.orion-lubricants.com
Source Michuzi

Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger