Home » » Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana amaliza ziara yake ya kikazi katika mikoa ya Ruvuma na Mbeya na baadae kupitia mkoa wa Njombe kukagua baadhi ya miradi mbalimbali na kazi za kijamii.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana amaliza ziara yake ya kikazi katika mikoa ya Ruvuma na Mbeya na baadae kupitia mkoa wa Njombe kukagua baadhi ya miradi mbalimbali na kazi za kijamii.

Written By JAK on Saturday, December 7, 2013 | 4:01 AM


 Gari aliyokuwa amepanda Katibu wa NEC,Siasa na mahusiano ya Kimataifa,Dkt Asharose Migiro ikiwa imepoteza muelekeo,kufuatia eneo hilo kukumbwa na utelezi mkubwa kutokana na mvua iliyokuwa imenyesha.Dkt.Migiro alikuwa kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana walipokuwa wakitokea Wilayani Makete kuelekea Wilaya mpya ya Wanging'ombe,mkoani Njombe mapema leo ambapo hata hivyo walifika salama na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii.
 Juhudi ya kulinasua gari hilo zikiendelea kufanyika.
Pichani Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa sambamba na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na wadau wengine wakitoka kutoa msaada wakati gari ya Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa iliponasa kwenye tope.
 Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro akiwa amesimama kando kando ya barabara akisubiri gari yake iliyokuwa kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,iondolewa mara baada ya kunasa kwenye tope,kufuatia eneo hilo kuharibika kutokana na mvua kunyesha na kusababisha utelezi mkubwa eneo hilo.
 Juhudi za kulinasua gari hilo zikiendelea.
 Eneo linavyoonekana
Gari ikiwa imekwishaondolewa kwenye eneo korofi tayari kwa kuendelea na msafara kutoka Wilaya ya Makete kuelekea Wilaya mpya ya Wanging'ombe,mkoani Njombe.Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC,ItIkadi na Uenezi,Nape Nnauye,Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro amemaliza ziara yake ya kikazi katika mikoa ya Ruvuma na Mbeya na baadae kupitia mkoa wa Njombe kukagua baadhi ya miradi mbalimbali na kazi za kijamii.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger