Home » » PINDA AHUDHURIA MAHAFALI YA YA CHUO KIKUU MZUMBE MJINI MOROGORO

PINDA AHUDHURIA MAHAFALI YA YA CHUO KIKUU MZUMBE MJINI MOROGORO

Written By JAK on Saturday, December 7, 2013 | 3:54 AM


 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Jaji Barnabas Samata  (kushoto) akimtunuku Shahada ya Udaktari wa Falsafa ya Chuo Kikuu hicho,  Mbunge  wa Viti Maalum Pindi Chana  katika Mahafali yaliyofanyika Chuoni hapo mjini Morogoro leo.
 Mbunge wa Viti Maalum, Pindi Chana  akishukuru baada ya kutunukiwa Shahada  ya Udaktari wa Falsafa ya Chuo Kikuu cha Mzumbe na Mkuu wa Chuo hicho, Jaji Barnabas Samatta  (wapili kulia) katika mahafali ya Chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo mjini Morogoro leo.   Wa nne kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na wasita kulia ni mkewe Mama Tunu Pinda akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Joel Bendera.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Mama Tunu Pinda wakopozi kwa furaha na Binti yao Janet Pinda  ambaye alipokea Shahada  ya Uzamili ya Uongozi katika Mifumo ya Afya kwenye Mahafali ya Chuo Kikuu cha Mzumbe yaliyofanyika Chuoni hapo mjini Morogoro leo.
  Mtoto wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Janet Pinda  (kulia) akipongezwa na wadogozake, Nasirika  Nyema (wapili kulia) na  Namsi Pinda (kushoto) baada ya kutunukiwa  Shahada ya Uzamili  ya Uongozi  katika Mifumo ya Afya kwenye Mahafali ya Chuo Kikuu cha Mzumbe mjini Morogoro leo.
  Mtoto wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda,  Janet Pinda,  akipongezwa na shangazi yake , Beatha Pinda Kaitira (kushoto) baada ya kutunukiwa shahada ya uzamili ya uongozi  katika mifumo ya afya kwenye mahafali ya chuo kikuu cha mzumbe mjini Morogoro December
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika mahafali ya Chuo Kikuu cha Mzumbe mjiniMorogoro  Desemba 6, 2013. Katikati ni mkewe Mama Tunu Pinda. Picha na PMO
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger