LEMA AKIMBIA MKUTANO WA KUITAKIA AMANI MKOA WA ARUSHA
Wadau wa amani wakiwa jukwaa kuu wakiwa wanafuatilia matukio mbali mbali ya maadhimisho ya kuutakia amani mkoa wa Arusha baada ya kukumbwa na matukio mbali mbali yaliotokea baada ya uchaguzi mkuu na mabomu kwenye kanisa la Joseph mfanyakazi olasit na Soweto mkutano ulioandaliwa na msajili wa vyama vya siasa na vyama vya siasa mkoani hapa na kufanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini hapa.
Mmoja wa washiriki akiwaonyesha viongozi na wananchi wa jiji la Arusha hawapo pichani waliohudhuria hafla hiyo bango lisemalo amani kwanza vyama baadae ujumbe ulioendana na siku hiyo mbele ya msajili wa vyama vya siasa jaji Francis Mutungi na mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo na viongozi wa vyama vya siasa na dini mkoani hapa.
Sehemu ya umati mkubwa wa wananchi na wakazi wa mkoa wa Arusha walioshiriki kuiombea amani mkoa wa Arusha wakifuatilia matukio mbali mbali yaliokuwa yakiendelea uwanjani
Mchungaji Christopher Mwakasege akiombea amani ya mkoa wa Arusha kwenye siku hiyo ya kusahau tofauti na matukio yaliotokea kwenye mkoa huu wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kwenye uwanja wa sheikh Amri Kaluta Abeid
Juu na chini wanaonekana viongozi mbali mbali wa serikali, vyama vya siasa na dini mkoani Arusha Pamoja na mgeni Rasmi Jaji Francis Mutungi Msajili wa Vyama vya siasa wakiwa kwenye maombi yaliokuwa yakiombwa na mwalimu na mchungaji Christopher Mwakasege kwenye uwanja wa sheikh Amri Kaluta Abeid.
Baadhi ya bendera za vyama vya Kisiasa na serekali zikipepea uwanjani hapo.
Umati wa Wana Arusha waliohudhuria katika mkutano huo kwa ajili kuitakia mema mkoa wa Arusha
Baadhi ya Wanahabari wakifuatilia kwa karibu.
Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia matukio kwa karibu.
Wanahabari wakiwa mzigoni.
Jaji Francis Mutungi Msajili wa Vyama vya siasa akiteta jambo na Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua akimpongeza mgeni rasmi kwa kazi nzuri aliyoianzisha,mara baada ya Mkutano huo.
Wadau mbalimbali akiwemo Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM Wilaya ya Arusha Ndg Victor Mollel (katikati aliyevaa sweta)
Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Fransis Mutungi amewataka wananchi wa Mkoa wa Arusha na Watanzania kwa ujumla kuepuka kuingiza ushabiki kwenye siasa kwani kufanya hivyo licha ya kuwa chanzo cha kuhatarisha amani wanaharibu lengo la fani hiyo ambayo ina umuhimu na faida kubwa katika jamii kama taratibu na misingi yake ikifuatwa na kuheshimiwa .
Akizungumza na wananchi na viongozi wa ngazi mbalimbali za Mkoa wa Arusha waliokusanyika katika uwanja wa Shekh Amri Abeid kuuombea mkoa wa Arusha amani Jaji Mutungi amesema amani ndio msingi wa kila kitu na haihusiani kabisa na siasa hivyo hakuna sababu ya watanzania kukubali amani iliyopo isivurugwe na watu wachache wanaosingizia siasa kwani wanaopenda amani ni wengi kuliko wanasiasa.
Wakizungumza katika hafla hiyo viongozi wa ngazi mbalimbali akiwemo Shekh Mkuu wa Mkoa Shabani bin Jumaa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Evengelisim Centre Eliud wamewaomba viongozi wa kisiasa na wanaotarajia kutafuta nafasi za uongozi kuwajengea wananchi utamaduni wa kuheshimu sheria na dola iliyoko madarakani kwani wakizoea kuvunja sheria watafanya hivyo hata uongozi ulioko madarakani ukibadilika .
Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw Magesa Mulongo amesema upo uwezekano wa kuendesha siasa, kudai haki na hata kukosoa na kutoa mapendekezo bila kuvuruga amani.
Wananchi hao wakiwa na viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo wa kisiasa ,viongozi wa dini na wa mila walikusanyika katika uwanja huo kuhubiri na kuuombea Mkoa wa Arusha amani unaoandamwa na heka heka za kisiasa ambazo zimesababisha kuyumba kwa uchumi.
Post a Comment