Home » » MTANZANIA ADAKWA NA MADAWA YA KULEVYA MACAU, CHINA

MTANZANIA ADAKWA NA MADAWA YA KULEVYA MACAU, CHINA

Written By JAK on Saturday, December 28, 2013 | 9:32 PM


Mwanamke wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 28 amekutwa na kilo 1.1 za madawa ya kulevya aina ya heroin alizokuwa amezihifadhi tumboni mwake,baada ya kukamatwa huko Macao, nchini China. Dawa hizo zenye jumla ya vidonge 66 vinakadiriwa kuwa na thamani ya dola za Kimarekani 137,720.

Mwanamke huyo alikuwa akisafiri kutoka Thailand akielekea Macao Jumanne iliyopita. Aliwaambia polisi kuwa alikuwa anaelekea Guangzhou ambao ni mji wa jimbo la Guangdong huko Chima.
Pichani ni mwanamke huyo wa Kitanzania (akiwa amefunikwa uso) aliyekamatwa na kilo 1.1 za heroin huko Macau. Hapo amepigwa picha na vidonge vyake wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari mjini Macau, Disemba 19, 2013.


Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger