Habari iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde toka jijini Arusha,inaeleza kuwa Ndege ya abiria aina ya Boeing 767 ya shirika la ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines) mchana huu imeshindwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kutoka na hitilafu iliyokuwepo Uwanjani hapo na kulazimika kutua kwa dharula kwenye Uwanja wa Mdogo wa Arusha.
Wataalam wa Ndege wapo eneo la tukio hivi sasa kutafakari namna watakavyoweza kuwashusha abiria hao na kutafuta namna ya kuweka sawa mambo ili Ndege hiyo iweze kuruka.
Ndege hiyo ilikuwa na abiria zaidi ya 200 na wafanyakazi 9. kabla ya kupaa tena ilibidi abiria wote wateremke, na kupunguzwa mafuta ili kupunguza uzito wa ndege hiyo. Abiria waliamuriwa kwenda kupandia ndege hiyo kwenye Uwanja wa Ndege wa KIA.
Globu ya Jamii inaendelea kufatilia kwa ukaribu tukio hilo,na tutaendelea kufahamishana kadri taarifa zitakavyokuwa zikitufikia.
Post a Comment