Pichani kulia ni aliyewahi kuwa Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006,Jokate Mwegelo akizungumza na baadhi ya Wanahabari (hawapo pichani) kutoka vyombo mbalimbali mapema leo Mikocheni jijini Dar kuhusiana na uzinduzi wa klabu yake iliyojulikana kwa jina la KIDOTI CLUB,Shoto ni mmoja waratibu,Mtangazaji wa East Africa Radio aitwaye Bhoke.
Mmoja wa Mashuhuda akitoa ushuhuda wake mara baada ya kujiunga kwenye klabu ya KIDOTI CLUB,kwa njia ya simu kwa kutuma neno KIDOTI kwenda namba 15678 na kuanza kupata taarifa mbali mbali kutoka kwake
katika kampeni hiyo ijulikanayo kwa jina la Kidoti Ng’aring’ari.
Baadhi ya wanahabari waliofika kwenye uzinduzi huo uliofanyika Mikocheni,jijini Dar.
========= ======== ========
Baada ya kutamba na mitindo ya nywele na nguo
aina ya Kidoti brand, msichana mwenye vipaji vingi hapa nchini, Jokate
Mwegelo ameanzisha klabu yake ijulikanayo kwa jina la Kidoti Club.
Akizungumza katika uzinduzi wa klabu hiyo jana,
Jokate alisema kuwa Kidoti Club ni tofauti na vilabu vingine kwani
katika ujio wake huo mpya, atakuwa anajihusisha na mambo mbali mbali
katika jamii hususani masuala ya urembo na mitindo. Jokate pia alizindua
aina mpya ya nywele zake za kisasa katika mtindo wa kidoti Brand.
Jokate
alisema kuwa kupitia klabu yake atakuwa anatoa ushauri mbali mbali
katika jamii na ikiwa pamoja na taarifa za muziki, filamu, wasanii
mbalimbali na nyinginezo kwa ajili ya rika tofauti. Alisema kuwa lengo
lake kubwa ni kupanua mtandao wake kwa jamii na anaamini watu wengi
watajiunga naye.
Kwa mujibu wa Jokate ambaye ni Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006, ili uwe mwanachama wa klabu hiyo, unatakiwa kutuma neno kidoti
kwenda namba 15678 na kuanza kupata taarifa mbali mbali kutoka kwake
katika kampeni hiyo ijulikanayo kwa jina la Kidoti Ng’aring’ari.
“Huu
ni mfumo wa kisasa katika kutoa taarifa mbali mbali kwa jamii,Beyonce
amefanya hivyo na kwa sasa hakuna mtu anayeingia katika shoo zake bila
kuwa mwanachama wa klabu yake, mimi pia naelekea huko kwani nitaweka
taarifa zangu mbali mbali na ili kupata lazima uwe mwanachama,” alisema
Jokate ambaye pia ni mtangazaji na mbunifu wa mavazi. Alisema kuwa pia ataendesha mashindano mbali mbali kwa wanachama wake na kutoa zawadi kwa washindi.
“Kama
unavyojua, lengo langu kubwa ni kutumia ujuzi na kipaji chake kwa
watanzania wote, nataka wafaidike na vipaji vyangu name kusimama
mwenyewe katika maisha bila ya kumtegemea mtu yoyote, natoa wito kwa
vijana wenzangu kuwa wabunifu katika kukabiliana na masuala mbali mbali
ya maisha,” alisema.
Post a Comment