Home » » WATANZANIA TUITUNZE AMANI TULIYONAYO-ROSE MUHANDO.

WATANZANIA TUITUNZE AMANI TULIYONAYO-ROSE MUHANDO.

Written By JAK on Tuesday, December 31, 2013 | 5:56 AM


Nyota mahiri wa nyimbo za injili,ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Facebook na Shikilia Pindo la Yesu,Rose Muhando akiimba huku akiwa amezungukwa na washabiki na wapenzi wa nyimbo za injili ndani ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid,jana jijini Arusha.Rose Muhando pia aliwaasa wakazi wa jiji hilo na kwingineko kuitunza amani ya nchi yetu tulionayo,kuonesha upendo na mshkamanno miongoni  mwetu kuhakikisha nchi yetu inabaki kuwa yenye amani daima dumu.

Tamasha hilo linaloandaliwa na kampuni ya Msama Promotions Ltd,liko kwenye mwendelezo wa uzinduzi wa tamasha la Krismasi kwa mikoa mitano kuelekea kuupokea Mwaka mpya,ambapo siku ya mwaka mpya tamasha hilo litafanyika mkoani Dodoma na kuwahusisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili ndani na nje ya nchi.
Nyota mahiri wa nyimbo za injili,ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Facebook na Shikilia Pindo la Yesu,Rose Muhando akiimba mbele washabiki na wapenzi wa nyimbo za injili ndani ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid,jana jijini Arusha.Tamasha hilo linaloandaliwa na kampuni ya Msama Promotions Ltd,liko kwenye mwendelezo wa uzinduzi wa tamasha la Krismasi kwa mikoa mitano kuelekea kuupokea Mwaka mpya,ambapo siku ya mwaka mpya tamasha hilo litafanyika mkoan Dodoma na kuwahusisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili ndani na nje ya nchi.
Sehemu ya wapenzi wa nyimbo za injili wakiwa kwenye tamasha hilo huku wakiwa na hisia ya kuguswa mno kupitia nyimbo mbalimbali zilizokuwa zikiimbwa na waimbaji mbalimbali waliokuwepo kwenye tamasha hilo liliofanyika ndani ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid hapo jana.
Mmoja wa waimbaji mahiri wa nyimbo za injili,Bone Mwaitege akiimba huku akiwa amezungukwa na mashabiki wake.
Pichani ni Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions inayyoandaa matamasha ya Pasaka na hili la Krismasi,Bwa.Alex Msama akiwashukuru wakazi wa jiji la Arusha kwa kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo,aidha amewataka wakazii wa jiji hilo kuhakikisha wanadumisha amani na upendo walionayo miongoni mwao,ili kuifanya nchi yetu iendelee kujiwekea historia ya kulinda,kutunza,kudumisha  na kuienzi amani yetu kwa nguvu zote.
Mwimbaji wanyimbo za kusifu na kuabudu,Upendo Nkone akiimba mbele ya wapenzi wa nyimbo za injili waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo lililopokelewa vyema jijini Arusha.
Mmoja wa waimbaji mahiri wa nyimbo za injili,Bone Mwaitege akiwaimbisha mashabiki wake.
Sehemu ya wapenzi wa nyimbo za injili wakiwa kwenye tamasha hilo huku wakiwa na hisia ya kuguswa mno kupitia nyimbo mbalimbali zilizokuwa zikiimbwa na waimbaji mbalimbali waliokuwepo kwenye tamasha hilo liliofanyika ndani ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid hapo jana.
The Voice a.k.a Vijana wa Acapela wakiwa jukwaani wakitumbuiza wakazi wa jiji la Arusha waliofika kwenye tamasha la muendelezo wa Krismasi kuelekea mapokeo ya mwaka mpya ndani ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha.
Kwaya ya kundi la The New Life Band wakitumbuiza jukwaani.
Upendo Kilahiro akiwaimbisha watazamaji wa tamasha hilo (hawapo pichani) 
Mmoja wa waimbaji mahiri wa nyimbo za injili kutoka nchini Zambia,Epfraim Sekeleti akiimba kwa hisia jukwaani,huku shangwe na vigeregere vya watazamaji vikilipuka kutoka kila kona ya uwanja.

Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger