Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu Serikali ameagiza
kumalizwa kwa migogoro ya mipaka baina ya Hifadhi ya Tarangire, Pori la Akiba
la Mkungunero na wananchi iliyodumu kwa muda wa takribani miaka kumi
hadi sasa. Nyalandu amewataka wananchi wa vijiji vinavyopakana na hifadhi
hizo kuacha kuvamia maeneo yaliyotengwa kisheria kwani kwa kufanya hivyo ni
kuleta migogoro isiyo ya lazima.
Mhe. Nyalandu alikuwa akiongea katika kikao maalum cha Kamati za Ulinzi na
Usalama za mikoa ya Manayara na Dodoma wilayani Babati mkoani Manyara
zilizokutana kwa ajili ya kujadili suluhu ya migogoro hiyo.
Aliongeza kusema kuwa serikali imedhamiria kumaliza mgogoro hiyo kwa
kuishirikisha jamii kwa upana zaidi huku akisisitiza kwamba Serikali itaendelea
kusimamia na kutekeleza Sheria ya Uhifadhi bila kumuonea mwananchi yoyote
na kwa kuzingatia haki za binadamu.
Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na Kamati
za Ulinzi na Usalama za Mikoa ya Manyara na Dodoma wakati wa kikao
maalum cha kujadili masuala ya migogoro ya mipaka katika Hifadhi ya
Taifa Tarangire na Pori la Akiba la Mkungunero wilayani Babati, Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Elaston Mbwilo akisitiza jambo wakati
wa kikao maalum cha Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Dodoma
na Manyara cha kujadili masuala ya migogoro ya mipaka katika Hifadhi ya
Taifa Tarangire na Pori la Akiba la Mkungunero wilayani Babati, Manyara.
Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi.
Sehemu wa wajumbe waliokutana katika kikao maalum cha Kamati za
Ulinzi na Usalama za mikoa ya Dodoma na Manyara cha kujadili masuala
ya migogoro ya mipaka katika Hifadhi ya Taifa Tarangire na Pori la Akiba
la Mkungunero wilayani Babati, Manyara.
Kutoka kulia: Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi, Mkurugenzi wa
Idara ya Wanyamapori Profesa Alexander Songorwa na KatibuTawala wa
Mkoa wa Dodoma Rehema Madenge wakifuatilia mada zilizowasilishwa
wakati wa kikao maalum cha Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya
Dodoma na Manyara cha kujadili masuala ya migogoro ya mipaka katika
Hifadhi ya Taifa Tarangire na Pori la Akiba la Mkungunero wilayani Babati,
Manyara.
Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na
Waheshimiwa Wabunge Zabein Mhita na Moza Abeid kutoka Dodoma
wakati wa kikao hicho.
Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na
wanahabari mara baada ya kikao hicho.
Post a Comment