Ujumbe wa Algeria umepata nafasi ya kutembelea machimbo ya Tanzanite Mererani
katika Kampuni ya TanzaniteOne ambapo walitembelea sehemu mbalimbali
ikiwemo za uzalishaji, usafishaji, na uchongaji madini ya Tanzanite.
Vilevile, wakiwa
Mkoani Kilimanjaro walipata fursa ya kutembelea Kiwanda cha kuzalisha mbolea
ya kupandia cha Minjingu ambapo walijionea namna mbolea hiyo inavyozalishwa
kwa kutumia masalia ya ndege aina ya Flamingo waliokuwepo eneo hilo miaka
mingi iliyopita.
Aidha, ujumbe huo ulipata fursa ya kutembelea mbuga za wanyama
katika bonde la ngorongoro ambapo wamehitimisha ziara yao nchini ya kujifunza na
kubadilishana uzoefu na nchi ya Tanzania katika sekta za gesi, mafuta,umeme na
madini.
Mkurugenzi Mkuu wa Migodi katika Wizara ya Nishati na Migodi ya Algeria Bw.
Bourroudj Mohamed Tawar (aliyenyoosha mkono) akiangalia mwamba uliotokana na
masalia ya ndege aina ya flamingo, yanayozalisha Mbolea ya kupanda ya Minjingu.
Mwenye koti jeupe ni Mkuu wa uzalishaji wa kiwanda cha Minjingu Bw. Inyana
Mwambete, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho Bw. Tosky Hans
na wa kwanza kulia ni Kamishna wa Madini Wizara ya Nishati na Madini Bw. Ally
Samaje.
Mtaalamu wa madini katika machimbo ya Kampuni ya TanzaniteOne Mererani
Bw. Damian Mansala akiueleza ujumbe wa Algeria namna mitambo ya kupeleka
wachimbaji ardhini na namna mtambo huo unavyosafirisha mchanga wa madini
uliochimbwa na kuusambaza katika hatua mbalimbali za uzalishaji wa madini ya
Tanzanite.
Kamishna wa Madini Wizara ya Nishati na Madini Bw. Ally Sameja akiuongoza
ujumbe wa Algeria kuondoka katika uwanja wa ndege wa Arusha , mara baada ya
kumaliza ziara Mkoani humo.
Meneja Mradi wa Kampuni ya TanzaniteOne Bw. Erenet Emmanuel Mtawali
(mwenye kofia nyekundu) akiueleza ujumbe wa Algeria namna mitambo ya
kusafisha na kuzalisha madini ya Tanzanite (haupo pichani) unavyofanya kazi.
Post a Comment