"Miaka michache tu wanajigamba, wanapiga kelele, lakini pia kwa kipindi hicho kifupi tayari wameanza mifarakano,Wafanye kazi kubwa kutufikia,"alisema Angellah Kairuki ambaye ni Mjumbe Baraza la Taifa la Umoja wa Wanawake (UWT), Angellah Kairuki.
Alisifu kwamba hadi kufika hapo, ni kutokana na mshikamano wa wanaCCM, na kuwataka kushikamana zaidi ili kurudisha majimbo yaliyopotea katika uchaguzi mkuu uliopita. "Wakati ni sasa,m mkono kwa mkono, nyumba kwa nyumba turudishe majimbo uliyopoteza..changamoto za kiamendeleo zipo, lakini haziwezi kutatuliwa kwa siku moja.
Cheers na Wanachama.
"Ndio maana Chama kina ilani kwa ajili ya kutekeleza vizuri mikakati ya maendeleo nchini,"aliongeza. Angellah alisema kwa muda ambao CCM ipo madarakani, imefanya mambo mengi na mfano ni mji huo mpya wa Mabwepande.
Alisema kwa muda mfupi mji huo umepiga hatua kubwa, na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imejipanga kikamilifu kutekeleza miradi ambayo mingine imeshaanza, ikiwa ni pamoja na mabweni ya wasichana yanayojengwa kwa kushirikiana na serikali ya Korea, barabara, madaraja, na mfumo wa maji safi na taka.
Aliwataka wajivunie mafanikio chini ya serikali ya CCM na kuyatangaza, na kutowapa nafasi wapinzaniaambao wamekuwa wakipiga kelele bila kuona mafanikio hayo. Aidha, aliwahamasisha kushiriki vizuri katika mchakato wa kupata katiba mpya, hususan wakati wa kura za maoni, kutetea misimamo ya Chama.
Aliwaasa kujipanga vizuri kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu kwakuchagua viongozi, wanaokubali kwenye jamii hodari na mchapakazi.
Post a Comment