Home » » WACHIMBAJI WADOGO TUNDURU WATEMBELEA MGODI WA MAST LTD KWA AJILI YA KUJIFUNZA NAMNA BORA YA UCHIMBAJI WA MADINI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA

WACHIMBAJI WADOGO TUNDURU WATEMBELEA MGODI WA MAST LTD KWA AJILI YA KUJIFUNZA NAMNA BORA YA UCHIMBAJI WA MADINI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Written By JAK on Monday, February 3, 2014 | 6:31 AM

 Kamishna Msaidizi wa Madini -Uendelezaji wa Uchimbaji Mdogo, Mhandisi Fredy Mahobe kutoka Wizara ya Nishati na Madini akifafanua namna  ya kuendesha uchimbaji salama wa madini kwa wachimbaji wadogo mara walipotembelea mgodi wa Minerals Access System Tanzania (MAST). Ziara hiyo ni moja ya mafunzo ya vitendo kwa wachimbaji wadogo waliohudhuria mafunzo yanayoendelea Tunduru mkoani Ruvuma.
 Mjiolojia Mwandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini Bw. Julius Sarota akielezea jinsi madini ya shaba yanavyoweza kutambuliwa kupitia kipande cha mwamba alichokishika.
 Mmoja wa wachimbaji wadogo ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiuliza swali kwa mwezeshaji Mjiolojia Mwandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini Bw. Julius Sarota (hayupo pichani)
 Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Kungulu Kasongi (aliyevaa shati jeupe) akiwaelezea wachimbaji wadogo namna uchorongaji wa miamba unavyofanyika mara wachimbaji wao walipotembelea mgodi wa Minerals Access System Tanzania (MAST) uliopo Tunduru, Ruvuma.
 Mtaalam wa kampuni ya MAST akionesha namna ya kuchoronga miamba kwa wachimbaji wadogo ( hawapo pichani). 
 Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Jones Mushi akionesha jinsi  uunganishaji wa mlipuko wa baruti unavyofanyika kwa wachimbaji wadogo (hawapo pichani) kwenye machimbo ya mgodi wa MAST uliopo Tunduru, Ruvuma.


 Kazi ya uunganishaji wa mlipuko wa baruti ikiendelea katika mafunzo ya wachimbaji wadogo wa madini wa Tunduru. 
 Wachimbaji wadogo wakiangalia shimo mara baada ya kulipuliwa na baruti.
 Mtaalam kutoka kampuni ya MAST Mhandisi Thomas Kato alielezea wachimbaji wadogo jinsi vifaa vya uchimbaji madini vinavyofanya kazi.
 Mhandisi  Heri Issa kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) akionesha moja ya mashine ya kuponda mawe inavyofanya kazi kwenye machimbo ya kampuni ya MAST. 
Kamishna Msaidizi wa Madini - Uendelezaji wa Uchimbaji Mdogo, Mhandisi Fredy Mahobe kutoka Wizara ya Nishati na Madini akifafanua namna bora ya utunzaji wa mazingira kwenye eneo la kutunzia mawetaka kwenye  machimbo ya kampuni ya MAST yaliyopo Tunduru, Ruvuma. 

Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger